Michezo

FC Barcelona watolewa jasho na Mamelodi Sundown ya Afrika Kusini (+video)

Klabu ya FC Barcelona usiku wa jana ilivaana na klabu ya Mamelodi Sundown ya Afrika Kusini kwenye mchezo wa kirafiki ambao ulikuwa na msisimko wa hali ya juu.

Image result for fc barcelona and mamelodi Sundown

Kikosi cha Barcelona kilikuwa na wachezaji wake karibia wote na kwenye mchezo huo walicheza wote kwa kubadilishana kipindi cha pili ambapo mchezaji wao tegemezi, Muajentina Lionel Messi aliingia kuitumikia klabu yake.

Licha ya kuonekana kuwa na ari na nguvu uwanjani kuwazidi Barcelona, Mamelodi walishindwa kuhimili mikiki mikiki ya Barcelona na kuruhusu magoli matatu huku wao wakiambulia goli moja la kufutia machozi.

Magoli ya Barcelona yalifungwa na Oesuman Dembele, Luis Suarez na Andre Gomes huku goli pekee la kifuta jasho la Mamelodi likifungwa na Sibusiso Vilakazi.

Soma zaidi kuhusu mchezo huo ambao umechezwa katika sherehe za kuadhimisha miaka 100 ya muasisi wa taifa hilo, Hayati Nelson Mandela. ->Bilionea amwaga kiasi hiki cha pesa kuileta Barcelona Afrika, na hii ndio timu itakayocheza na wababe hao wa soka duniani

Tazama magoli yote hapa chini:

https://youtu.be/aNsEyo5go3Y

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents