Michezo

Bilionea amwaga kiasi hiki cha pesa kuileta Barcelona Afrika, na hii ndio timu itakayocheza na wababe hao wa soka duniani

Ukiambiwa watu barani Afrika wana pesa usikatae kwa vile wewe hauna, unaambiwa mmiliki wa klabu ya Mamelodi Sundown ya nchini Afrika Kusini, Bilionea Patrice Motsepe amejitosa kulipia kiasi cha dola milioni $7.9 sawa na Tsh bilioni 18 za kulipia gharama za kuileta klabu ya Barcelona nchini Afrika Kusini.

Patrice Motsepe

Tayari mazungumzo yameshafanyika na Barcelona wamethibitisha taarifa hizo kupitia website yao ambapo watacheza mechi ya kirafiki na klabu ya Sundown Mamelodi Mei 6, 2018.

Mbali na mchezo huo, Barcelona pia watapamba sherehe ya kutimiza miaka 100 ya aliyekuwa kiongozi wa taifa na mpambanaji wa ubaguzi wa rangi hayati Nelson Mandela.

Mchezo huo unakuwa ni wa 21 kwa klabu ya Barcelona kucheza wakiwa kwenye ardhi ya Afrika na mara yao ya mwisho kucheza barani Afrika ni mwaka 2007 ambapo walicheza na klabu ya Pretoria ya nchini Afrika Kusini na walishinda goli 2-1 .

Hata hivyo, Mei 6 klabu ya Sundown Mamelodi ilikuwa na mchezo wa klabu bingwa dhidi ya Horoya AS ya Guinea Conakri, na tayari CAF wametangaza kuupeleka mbele mchezo huo hadi Mei 22, 208.

Kikosi cha Barcelona kitakuja na mastaa wake wote akiwemo Lionel Messi, Suarez, Dembele, Coutinho na wengine wote.

Viingilio vya mchezo kati ya Barcelona na Mamelodi Sundown ni kuanzia  randi 40 sawa na tsh 7,500 na tiketi za VIP zitauzwa kati ya randi 350 sawa na tsh 64,500/= hadi randi 550 sawa na tsh 101,000/=.

Soma zaidi taarifa ya kutoka kwenye website ya Barcelona – Barça to play in the Mandela Centenary Cup in South Africa on May 16

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents