Burudani

Femi One aeleza kuhusu ‘Zaga Zaga’ na sababu za kumshirikisha Mejja

By  | 

Rapper Femi One kutoka nchini Kenya, amefunguka kuhusu wimbo wake mpya wa ‘Zaga Zaga’ na sabau za kumshirikisha Mejja kwenye ngoma hiyo.

Akiongea na Bongo5, rapper huyo wa kike ambaye yupo chini ya lebo ya Kaka Empire, amesema kuwa ngoma hiyo inamliwaza mtu anapokuwa na matatizo na pia ilikuwa ndoto yake ya muda mrefu kufanya kazi na Mejja.

“Kufanya kazi na Mejja imekuwa ndoto yangu ya muda mrefu, na wakati alipokubali kufanya kazi na mimi ilikuwa ni ndoto ya kweli,” amesema Femi.

“Zaga Zaga ni wimbo mzuri ni unaenda kwa mtu yeyote anayetaka kuwa na wakati mzuri baada ya mawazo mengi. Watu wangu wote wa Eastlando ukiskia hii ngoma weka shida zako kando,” ameongeza.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments