Burudani ya Michezo Live

Fid Q – August 13!! Bongo5 Exclusive

Fid QNi msanii pekee ambaye amechelewa kutoa albam yake ambayo imekuwa ikisubiriwa sana na mashabiki wa muziki kizazi kipya, Fid Fareed Q ama Fid Q au Ngosha The Don kama wengi ambavyo wamekuwa wakimuita.

Fid QNi msanii pekee ambaye amechelewa kutoa albam yake ambayo imekuwa ikisubiriwa sana na mashabiki wa muziki kizazi kipya, Fid Fareed Q ama Fid Q au Ngosha The Don kama wengi ambavyo wamekuwa wakimuita.

Kila singo ya msanii huyu ambayo amekuwa akiitoa imekuwa ikifanya vizuri katika chati mali mbali hapa nchini kuanzia ‘huyu na yule, Fid Q.Com, Chagua Moja, Mwanza Mwanza’ na sasa ametoka rasmi na jiwe lake la kufa mtu liitwalo ‘August 13′ ikiwa ni tarehe na mwaka aliozaliwa.

Ni wimboo ambao utapatikana katika albam yake ambayo iko njiani kuwafikia mashabiki wake, wenye kiu dhidi ya Fid Q, ambaye anasifika kwa kuwa na sifa ya kuandika mashairi yenye kumkuna msikilizaji yoyote.

Wimbo wa August 13, Fid amejaribu kuelezea maisha yake tangu alipoanza masuala ya muziki, na humo ndani amemshirikisha msanii Juma nature upande wa Chorus na Salama Jabiry kwenye Intro, wakati Prodyuza P-Funk Majani hakutaka kufanya mzaha kabisa katika upande wa Biti ambapo amekamua ile kinoma.

Iwapo utasikia ngoma hii hutasita kukubaliana na uwezo alio nao kijana huyu katika ubunifu, na uandaaji wa mashairi, suala zima hapa ni kukaa mkao wa kula kusubiri kuona ni nini alichokuwa akikiandaa kwa muda wote ambao amekuwa kimya.

CLICK PLAY TO LISTEN – BOFYA ALAMA YA PLAY KUSIKILIZA
FID-Q FEATURING JUMA NATURE: AUGUST 13

{play}august 13_fidq.mp3{/play}

 
Source: Bongo5

{mos_sb_discuss:6}

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW