Michezo

Francis Cheka afunguka mazito baada ya kutwangwa na Mswisi

Baada ya kupokea mkong’oto kutoka kwa Mswisi Enes Zecirevic usiku wa kuamkia leo Jumapili, bondia Francis Cheka amefunguka sababu za kupoteza pambano hilo.

Francis Cheka kulia akirusha konde

Cheka ambaye alipigwa kwa pointi za majaji 3-0 kwenye pambano hilo la raundi nane la uzani mwepesi wa juu (kg 81) lililofanyika mjini Geneva, amesema pambano hilo alishindwa kwa pointi za ugenini kwani ilitakiwa ashinde kwa Knock Out.

Nisingeweza kushinda kwa pointi, nilijua matokeo yale baada ya kumaliza raundi zote. Siku zote unapocheza ugenini na kumaliza raundi zote ni vigumu kupewa ushindi dhidi ya mwenyeji, ndivyo ilivyokuwa hata na kwangu.

“Nimeumizwa kuharibu rekodi yangu, lakini sijashangazwa na kupigwa kwa pointi kwani ni ushindi ambao yoyote anaweza kupewa,” amesema Cheka kwenye mahojiano yake na Gazeti la Mwananchi.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents