Michezo

Fred wa Man U atapata jeraha akifanya mazoezi na timu yake ya Brazil

Kiungo wa kati wa Brazil Fred ambaye kwa sasa amesainiwa na klabu ya Manchester United amepata jeraha katika kifundo chake cha mguu katika mazoezi kabla ya kuanza kwa kombe la dunia.

Fred amepata jeraha katika kifundo chake cha mguu katika mazoezi kabla ya kuanza kwa kombe la dunia.

Daktari wa timu ya Brazil Rodrigo Lasmar alilitaja jeraha hilo lililotokea mjini London kuwa lenye maumivu makali katika mguu wake.

“Kwa sasa ni mapema mno kusema chochote kuhusu hali yake. Siku ya Ijumaa tutaangalia tujue kitakachofanyikana kuamua iwapo tunahitaji kufanya uchunguzi wowote ama la,” alisema daktari huyo.

Brazil inaanza kampeni yake ya kombe la dunia dhidi ya Switzerland tarehe 17 mwezi Juni.

Washindi hao mara tano wa kombe la dunia baadaye watacheza katika kundi E dhidi ya Costa Rica na Serbia nchini Urusi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents