Fredrick Sumaye adai wanaohama vyama ni kuchezea fedha za wananchi na ufisadi

Waziri Mkuu mstaafu na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ukanda wa Pwani, Fredrick Sumaye amedai wabunge na madiwani wanaohama vyama na kupelekea uchaguzi kufanyika tena ni matumizi mabaya ya fedha za wananchi na ufisadi pia.

Mwanasiasa huyo akizungumza na kituo cha runinga cha Azam amesema mtu kuhama chama kimoja kwenda kingine haina shida lakini mtu anapohama labda kwa kushawishiwa au kwa sababu za maslai binafsi si sawa.

“Kama haya yanayotokea ni kwa sababu ya matumizi ya madaraka ama matumizi ya fedha hili jambo tulikemee sote,” amesema.

“Huwezi kutoka mbunge ama diwani kutoka Chadema/CUF ukaingia CCM halafu wakakuteua uende kwenye eneo lile lile, hii ni kuchezea fedha za wananchi kwa sababu ni kodi za wananchi, huo ni usifadi mkubwa,” amesisitiza.

Kwa kipindi cha mwaka jana wabunge watatu walijiuzulu na kuhamia vyama vingine, waliojiuzulu ni Lazaro Nyalandu, Maulid Mtulia,  Dkt. Godwin Mollel, pia kumekuwa na idadi kubwa ya madiwani wanaohama vyama.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW