Habari

Gavana wa Minnesota, Marekani ahofia Corona ”Waandamanaji hawakai mbalimbali, hawavai barakoa”

Maandamano makubwa yanayofanyika kote nchini Marekani baada ya mmarekani mweusi George Floyd kufa mikononi mwa polisi katika jimbo la Minnesota yamezidi kuenea katika miji 25 ikiwemo Minneapolis, Philadelphia na Los Angeles na kuibua wasiwasi kuhusu afya ya jamii.

Hofu iliyopo ni kwamba makundi makubwa ya waandamanaji huenda yakasababisha ongezeko la maambukizi ya virusi vya corona.

Baadhi ya viongozi wametoa wito kwa watu kuzingatia utulivu katika maeneo ambapo waandamanaji wenye hasira walivunja maduka na kuharibu magari ya polisi katika siku za hivi karibuni, viongozi hao pia wamegawa barakoa na kuwatahadharisha waandamanaji kwamba wanahatarisha maisha yao.

Hapo jana, gavana wa jimbo la Minnesota Tim Walz alielezea kuwa waandamanaji wengi hawazingatii maagizo ya kukaa mbalimbali na wala hawavai barakoa tofauti na ilivyokuwa mwanzoni mwa wiki.

Maandamano hayo yanafanyika wakati ambapo hatua za kulegeza karantini zimeanza kuchukuliwa katika miji mingi nchini Marekani.

New York, Atlanta na maeneo mengine yamekuwa yakishuhudia ghasia huku Ikulu ya Marekani ikiwekewa katika hatua ya kusalia ndani kwa muda mfupi.

Aliyekuwa afisa wa polisi katika eneo la Minneapolis ameshtakiwa kwa mauaji kutokana na kifo hicho.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents