Moto Hauzimwi

George Weah kukalia kiti cha Urais Liberia leo

Rais mteule wa Liberia George Oppong Ousman Weah ambaye pia amewahi kuwa mchezaji bora wa soka wa dunia, anatarajiwa kuapishwa leo kuwa Rais kamili wa nchi hiyo.

Weah ambaye alishinda kiti hicho mwezi uliopita atakuwa Rais wa 25 wa Liberia akichukua mikoba ya Rais Ellen Johnson Sirleaf ambaye amekalia kiti hicho kwa miaka 12.

Tukio hilo ambalo linasubiriwa kwa hamu kubwa na wananchi wa Liberia pamoja wa wadau wa soka duniani, litafanyika katika uwanja wa mpira wa Samuel Kanyon Doe majira ya saa sita mchana kwa saa za Afrika Mashariki.

Hii ni historia fupi ya George Weah.

Raisi Mteule wa Liberia 🇱🇷 ;

Senator: wa bunge la Liberia 2015

African Footballer of the (1989, 94, 95)

UEFA Champions League Top Scorer: 1994 – 15

1995 Ballon d’Or winner, FIFA World Player of the Year: 1995

1996 FIFA Fair Play Award

IFFHS African Player of the Century: 1996

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW