Habari

Ghasia zaibuka upya Nigeria, Ighalo wa Manchester United augana na raia kulaani vikali (+Video)

Majengo yamechomwa moto na kumeripotiwa kwa milio ya risasi katika miji mikubwa ya Nigeria wakati wa maandamano.

Shirika la kimataifa la Amnesty limesema watu wapatao 12 waliuawa na polisi na wanajeshi siku ya Jumannne.

Jeshi la Nigeria limekanusha ripoti hiyo na kudai kuwa ya uongo,waliandika katika kurasa ya Twitter.

Mamlaka iliweka amri ya kutotoka nje lakini baadhi walipuuzia agizo hilo.

Waandamanaji dhidi ya polisi wamekuwa barabarani kwa kipindi cha wiki mbili sasa.

Waandamanaji

Waandamanaji wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii kuhamasisha kampeni yao dhidi ya kikosi maalum cha polisi kinachojulikana kama Sars.

Rais Muhammadu Buhari alikisitisha kikosi hicho Oktoba 11. Lakini waandamanaji wameendelea na maandamano wakitaka mabadiliko zaidi katika vikosi vya usalama, pamoja na kubadilisha utendaji wao wa kazi.

Watu walioshuhudia milio ya risasi wameiambia BBC kuwa waliwaona jinsi polisi walivyokuwa wanamimina risasi Jumanne jioni.

Moshi mkubwa ulionekana juu ya anga la Lagos Jumatano
Moshi mkubwa ulionekana juu ya anga la Lagos Jumatano

Jumatano, baadhi ya majengo yalichomwa moto mjini Lagos na polisi waliweka zuio barabarani.

Kituo cha Televisheni Nigeria chenye uhusiano na chama tawala kilichomwa moto.

Polisi kutoka maeneo mbalimbnali walipiga risasi hewani ili kuwatawanyisha waandamanaji, mwandishi wa BBC Nduka Orjinmo anaripoti kutoka mji mkuu wa Abuja.

Aliripoti pia kuna nyumba zilivamiwa na kuibiwa kwa viongozi kadhaa wa kijadi.

Nini kilitokea Lagos?

Walioshuhudia wanasema watu wasiokuwa na sare walipiga risasi kwenye mkusanyiko wa waandamanji wapatao 1,000 siku ya Jumanne.

Kabla ya risasi kuanza kufyatuliwa, askari waliweka zuio barabarani , mwandishi wa BBC Nigeria Mayeni Jones anaripoti. Waandamanaji walionesha moja kwa moja kile kinachoendelea kwa kuweka video kwenye mitandao ya kijamii.

Ramani inayoonesha mahala lilipotokea tukio la ufyatuaji wa risasi Lagos:

Ramani inayoonesha ufyatuaji wa risasi lagos

Shahidi ambaye hakutaka jina lake litajwe aliambia BBC kwamba muda mfupi kabla ya saa moja wanajeshi walikongamana na kuanza kuwafyatulia risasi waandamanaji waliokuwa wakiandamana kwa amani moja kwa moja.

”Walikuwa wakifyatua risasi na kutukaribia . Zilikuwa ghasia. Mtu mmoja alipigwa risasi mbele yangu na kufariki papo hapo”, alisema.

Mashahidi wanne waliambia Reuters wanajeshi waliwafyatulia risasi waandamanaji.

Mmoja wao Alfred Ononugbo , mwenye umri wa miaka 55 alisema: Walikuwa wakifyatua risasi katikati ya waandamanaji . Niliona risasi zikiwapiga watu wawili.

Gazeti la Premium Times liliwanukuu mashahidi wakisema kwamba takriban watu 12 waliuawa. Katika ujumbe wa Twitter,Shirika la Amnesty International Tawi la Nigeria lilisema limepokea ushahidi wa kweli lakini unaogofya kuhusu utumizi wa nguvu kupitia kiasi uliosababisha vifo vya waandamanaji katika lango la Lekki mjini Lagos.

Msemaji wa Amnesty International Isa Sanusi baadaye alisema: Watu waliuawa na vikosi vya usalama katika lango la makaazi ya Lekki tunajaribu kuchunguza ni wangapi.

Waandamanji wamepuuza amri ya kutotoka nje Lagos

Asubuhi ya leo katika daraja refu la Lekki-Ikoyi lilichomwa moto usiku.

Wafanyabiashara kadhaa walivunjiwa majengo yao na biashara zao kuharibiwa.

Shughuli mbalimbali zilisitishwa katika miji mbalimbali na vijana tu wanaoandamana kwa miguu, hakuna magari yanayopita.

Wanigeria nchini Kenya wakiandamana nje ya ubalozi a Nigeria mjini Nairobi Jumatano
Wanigeria nchini Kenya wakiandamana nje ya ubalozi a Nigeria mjini Nairobi Jumatano

Maafisa wanajibu vipi?

Gavana wa Lagos Babajide Sanwo-Olu alisema watu wapatao 25 walijeruhiwa, na kuongeza kuwa wanafanya uchunguzi kuhusu hilo na mtu mmoja tu ambaye alifariki ili wanachunguza pia chanzo cha kifo chake kama kinahusiana na maandamano.

Jumatano alitaka bendera kushushwa katika majengo ya serikali na kusitisha shughuli za serikali kwa kipindi cha siku tatu.

Rais Buhari hakuzungumzia kufyatuliwa kwa risasi ila amewataka watu wawe watulivu na wavumilivu na waelewa wakati jitihada za mabadiliko zikiwa zinafanyika.

Hali ikoje katika Mataifa ya kigeni?

Maandamano yamefanyika Uingereza, Afrika Kusini na Kenya dhidi ya polisi wakatili Nigeria,wakati maafisa katika maeneo hayo wakilaani matukio hayo.

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres amewataka polisi kukabiliana na maandamano hayo kwa amani ili kuzuia ghasia zaidi.

Aliyekuwa waziri wa masuala ya kigeni nchini Marekani Hillary Clinton amemtaka rais Buhari na jeshi kuacha kuwaua vijana wanaoandamana wa vuguvugu la #EndSARS “.

Na aliyekuwa makamu wa rais nchini Marekani ambaye ndio mpinzani mkuu wa rais Donald Trump katika uchaguzi wa mwezi ujao Joe Biden – pia ametoa wito kwa mamlaka kusitisha ghasia dhidi ya waandamanaji.

Na anayewania urais Marekani Joe Biden ameitaka mamlaka ya Nigeria kusitisha vurugu hizo za maandamano.

https://www.instagram.com/tv/CGorH1zhbrD/

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents