Habari

Glady awa Miss Tanzania UK 2007

Mrembo Glady AnthonyMrembo Glady Anthony anayechukua fani ya sheria hapa London, ametwaa taji la mrembo wa Tanzania Uingereza ‘Miss Tanzania Uk 2007′ shindano lililofanyika kwenye Ukumbi wa La Royale, uliopo Tottenham na kuhudhuriwa na halaiki kubwa ya Watanzania wanaoishi hapa.



Mrembo Glady AnthonyMrembo Glady Anthony anayechukua fani ya sheria hapa London, ametwaa taji la mrembo wa Tanzania Uingereza ‘Miss Tanzania Uk 2007′ shindano lililofanyika kwenye Ukumbi wa La Royale, uliopo Tottenham na kuhudhuriwa na halaiki kubwa ya Watanzania wanaoishi hapa.


Glady anaesomea sheria mwaka wa kwanza, alionekana kuwa na uzoefu mkubwa wa kulimiliki jukwaa, alishinda taji hilo na kujipatia kitita cha paundi 1,000 sh2.8m za Tanzania na kupata tiketi ya kushiriki shindano la Miss Tanzania baadaye Septemba.


Attu Mynah msomi wa Chuo Kikuu cha Edinburgh, Scotland anaesomea miundombinu kwa njia ya komputa, alishika nafasi ya pili na kujipatia pauni 600 (sh1.5m). Shindano hilo limedhaminiwa na Kampuni ya Middle East Cargo, Karibu Salon, CRDB Bank chini ya Tanzanite Account na Coce .


Katika shindano hilo lililokuwa chini ya kampuni ya Geraton Promotion, nafasi ya tatu ilishikwa na Rachael Mzava aliyepata paundi 400 (sh1m) ambaye pia anasomea masuala ya televisheni na utangaza katika chuo kikuu cha Thems Valley kilichopo Ealing Brodway hapa London.


Nafasi ya nne ilishikwa na Nancy na nafasi ya tano ililikwenda kwa Nzala Pemba, katika shoo hiyo iliyopambwa na msanii Juma Nature na Profesa Haruna.


Shindano hilo lililohudhuliwa na Watazamaji wengi kuliko onesho lolote liliwahi kufanyika la Watanzania katika miaka ya hivi karibuni, mgeni rasmi alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mwanaidi Maajar Sinare, Mbunge wa Maswa, John Mimose Cheya.


Wengine ni Mama Radhia Msuya ambae ni Mkuu wa utawala wa Ubalozi, Hashim Lundenga aliyekuwa jaji mkuu akisaidiwa na Amos Msanjila ambaye ni Afisa Ubalozi na Rahma Aziz mtangazaji wa zamani wa Televisheni ya CTN Tanzania.


Kwa mujibu wa Lundenga, mshindi wa kwanza, Glady na Atu ndiyo watakaokwenda Tanzania kushiriki mashindano ya kumtafuta mrembo wa Tanzania, Mkurugenzi wa Geraton Promotion, Gerald Lusingu alisema hivi sasa wanaelekeza kwenye maandalizi ya kuwaandaa warembo hao kwenda Tanzania kushiriki mashindano ya Miss Tanzania.


“Kikubwa kwamba tumefanya shindano na tumejifunza mengi naamini mwakani tutaweza kufanya mambo mazuri zaidi ya onesho tutalibolesha,” alisema Lusingu.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents