Burudani ya Michezo Live

Godzilla aitaja sababu ya kwanini ngoma za hip hop hazina video nyingi kali kama za Bongo Flava

Rapper Godzilla aka Zizi anaamini kuwa misimamo ya wasanii wengi wa hip hop Tanzania ndio chanzo cha wao kutokuwa na video nyingi nzuri ukilinganisha na zile zinazofanywa na wasanii wa Bongo Flava.

Godzilla

Zilla ameiambia Bongo5 kuwa wasanii wa Bongo Flava wako tayari kujishusha hata kwa kupiga magoti kwa mtu mwenye fedha ambaye humpa fedha za kufanya video kali. Amesema kuwa kitu kama hicho hakipo kwa wasanii wengi wa hip hop ambao wameamua kufa na tai shingoni kama wajerumani au kwa lugha nyingine ni ‘maskini jeuri’.

Rapper huyo wa Salasala amedai kuwa video nyingi za wasanii wa kuimba zimefadhiliwa na mameneja wenye fedha aka mapapaa ambapo baadhi yao malipo yao ni kutajwa tu jina kwenye wimbo. Ameeleza kuwa rappers wengi hushindwa kukubaliana na masharti magumu ya mapapaa hao na hivyo kwa fedha zao wao wenyewe huwawia vigumu kuwekeza fedha nyingi kwenye video na kwamba sio wote wanapata show zinazowalipa vizuri.

Je unakubaliana na mawazo ya Godzilla?

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW