Technology

Utafiti: Wapenzi wanaotumia muda mwingi kwenye Twitter wana nafasi kubwa ya kuchepuka au kuachana

Facebook imekuwa ikilaumiwa kwa kusababisha kuvunjika kuvunjika kwa mahusiano, lakini Twitter nayo imebainika kuwa hatari katika uhusiano pia.

girl-tweeting

Kutweet sana husababisha malumbano hasa kuhusiana na muda mtu anatumia kwenye mtandao huo wa kijamii pamoja na wivu kwa mwenza anayejiuliza mwenzie anachat na nani. Kwa mujibu wa utafiti, wapenzi walio active zaidi kwenye mtandao huo wana hatihati ya kutokuwa waaminifu na inaweza kusababisha kuvunjika kwa uhusiano.

Mwanafunzi wa PhD, Russell Clayton wa chuo kikuu cha Missouri-Columbia aliwafanyia utafiti watumiaji 580 wa Twitter kuanzia miaka 18 hadi 67 kwa kutumia questionnaire za mtandaoni. Clayton alichambua tweets za kila mtu aliyeshiriki kabka ya kuwauliza maswali kuhusu uhusiano wao.

Alipima muda waliotumia kwenye, migogoro iliyozuka kutokana na matumizi yao na athari zilizotokea kwenye uhusiano wao. Alibaini kuwa wapenzi hujikuta wakilumbana kuhusiana na muda wanaotumia kwenye mtandao huo na pia jinsi ambayo wanakuwa marafiki na watu wengine.

“Watumiaji wa mara kwa mara wa mtandao huo walio kwenye uhusiano wa kimapenzi wanaweza kuona kwamba migogoro inayohusiana na Twitter inaweza kusababisha matatizo makubwa kiasi cha kusababisha usaliti nau talaka,” alisema Clayton. Hata hivyo ripoti yake ilidai kuwa tafiti zaidi zinahitaji kuona kama matatizo kama hayo yapo kwenye mitandao mingine Instagram.

Chanzo: Daily Mail

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents