Burudani

‘Grateful’ ya Dj Khaled yagonga Gold sokoni

By  | 

‘The Grateful’ ya Dj Khaled inazidi kuchanja mbuga sokoni.

Albamu hiyo imefikisha mauzo ya Gold sokoni, ikiwa na maana tayari imeshauza kopi laki tano tangu ilipotoka Juni 23 ya mwaka huu.

Kutokana na hatua hiyo chama cha Recording Industry Association of America (RIAA) kimemkabithi cheti rapper huyo. “Fan luv thank you GRATEFUL,” ameandika Khaled kwenye mtandao wake wa Twitter.
Nyimbo nyingine ambazo zinapatikana kwenye albamu hiyo mpya na zimeuza kopi laki tano ni ‘Shining aliyomshirikisha Beyoncé na Jay Z, ‘Wild Thoughts’ aliomshirikisha Rihanna na Bryson Tiller.

Wakati huo huo wimbo wa ‘I’m The One’ ambao pia unapatikana katika albamu hiyo ndio umeuza kopi nyingi zaidi ikiwa ni zaidi ya milioni tatu na kupatiwa cheti cha 3x platinum.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments