Habari

Habari ndio hiyo!

AY na MwanafalsafahUjio wa Albam ya pamoja baina ya msanii Ambewene Yessaya a.k.a AY na Hamisi MwinJumaa a.k.a Mwanafalsafah umonekana kuwa ni wa kihistoria kwani ni nadra sana kwa wasanii wa kibongo kufikia maamuzi kama yaliyofikiwa na vijana hawa.

AY na Mwanafalsafah

 

Ujio wa Albam ya pamoja baina ya msanii Ambewene Yessaya a.k.a AY na Hamisi MwinJumaa a.k.a Mwanafalsafah umonekana kuwa ni wa kihistoria kwani ni nadra sana kwa wasanii wa kibongo kufikia maamuzi kama yaliyofikiwa na vijana hawa.

 

Kila mmoja kati yao amewahi kufanya vizuri katika soko la muziki wa kizazi kipya hapa nchini kwa kuweka albam ya ukweli katika soko la muziki nchini ambapo Mwanafalsafah alitinga sokoni kwa mara ya kwanza kwa kishindo mara alipotua na Albam yake ‘Mwanafalsafani’ iliyokuwa na ‘hit’ kama vile ‘ingekuwa vipi, mabinti, showtime n.k, wakati mtu mzima A To Thah….alitimba nae kwa mara ya kwanza na Albam yake ya kwanza iliyokwenda kwa jina la ‘Raha Kamili’ ambayo ilishika na ngoma kama ‘Raha tu (rmx) aliyoshirikiana na Complex(RIP), Safi hiyo akiwa na Mwanafalsafah, Ray C na Banana, Raha Kamili n.k.

 

Hawakuishia hapo wakali hawa baada ya muda kidogo wakatua sokoni na albam zao nyingine ambapo Binamu alikurupuka na ‘Toleo Lijalo’ ambayo ilikuwa na Mawe kama vile ‘Alikufa Kwa Ngoma ambayo iliweza kuchukua tuzo ya wimbo bora wa Hip Hop, wanapendana akiwa na mtoto wa kizaramo Dully Sykes na nyinginezo kali zaidi.

 

Ambwene akajitoa tena hadharani na Albam yake ya pili ambayo na hii ni baada ya kupata mafanikio kiaina katika albam yake ya kwanza, ‘Hisia Zangu’ ndio albam yake ya pili ambayo iliweza kufanya vizuri nayo kwa kuwashika mashabiki na mikono kama vile ‘Binadamu, nipe nikupe, Yule n.k.

 

“Kuandika mashairi ni moja kati ya mchezo ambao naufurahia zaidi That’s Why siwezi kuacha kufanya albam nzuri kila ambapo mashabiki wangu wanahitaji kitu kipya kutoka kwangu, ‘Unanitega’ ndio albamu yangu ya mwisho kuiweka katika soko na inaweza kuonekana jinsi ilivyoweza kufanya vizuri kwa kuwa na mipini kama vile ‘Unanitega, Hawajui, na nyingine nyingi ambazo sijatoka nazo kwa sababu maalum na za kimsingi kabisa.

 

Habari ndio hiyo Albam
Maamuzi ya wakali hawa kufanya albam ya pamoja yalizuka baada ya kila mmoja kujiengua kwenye kundi la East Coast kwa sababu alizoona zinamsukuma kumwagana na kundi hilo fasta, licha ya kuachana na kundi hilo, maoni ya wadau na wasambazaji wa kazi mbali mbali za sanaa kugundua kuwa wakivikutanisha vichwa hivi viwili yawezekana kafanyika muziki wa ukweli na wenye kuikonga jamii kwa ujumla.

 

“Maoni ya wadau na wasambaji kwa pamoja baada ya kutoka east coast wakagundua tu Mimi na AY tukifanya albam ya pamoja itakuwa ni sababu moja wapo ya kuitoa sanaa ya muziki wa kizazi kipya na kuipeleka katika levo nyingine, jambo ambalo naamini hawatayajutia maoni yao hayo kwani mpaka sasa albam imeshakamilika na hatukufanya nyimbo tu bali tumengeneza ‘Hit’ tupu” kwa ngebe na majigambo alisema Fa.

 

Albam ina Jumla ya Nyimbo kumi ambazo zote ni kali, pia wameshirikishwa vinara kibao wa muziki wa ndani na nje ya Tanzania, wakiwepo Chameleon, Tallia, Q-Chief, Lady Jay Dee, Mangwea na wengine baadhi.

 

Katika mawe kumi ambayo wamerekodi wakali hao ni jiwe moja tu ambalo liko hewani nalo ni ‘Asubuhi’ ambalo wamemshirikisha mkali Q-Chief, wakati wimbo unaoibeba albam hiyo tayari umeshafanyiwa Video na Kampuni ya Visual Lab na Kijana Adam Juma kinachosubiriwa kutupwa kideoni tu Fasta.

 

Video ya wimbo wao ambao unaendelea kubamba katika vituo na kumbi mbali mbali za burudani nchini ‘Asubuhi’ utatarajiwa kuonekana kwenye luninga hivi punde kwa nao umeshakamilika ukiwa na hadhi za video za kimataifa.

 

Walizitaja baadhi ya ngoma ambazo zitapatikana katika albamu yao ‘Habari ndio hiyo’ nazo ni ‘Asubuhi, Bounce, nangoja ageuke, Habari ndio Hiyo, We Do, Binamu, Usijarubu, Fungua Champaigne, Umejuaje? na Kula kwa macho’ kazi zikiwa zimwfanywa na Maprodyuza mahiri waliochipukiwa kwa kasi akiwemo Hermy B, Marco Chali Lamar “Nasika furaha sana kushiriki katika albam ya Mwanafalsafah na AY hii inaonesha kuwa Mabro wananifil mimi na kazi yangu ninayoifanya Thanx God” alisema prodyuza mdogo sana kiumri mwenye kufanya kazi ambazo halingani nazo almaarufu kwa jina la Lamar.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents