Michezo

Haji Manara ampa somo Jamal Malinzi

Aliyekuwa msemaji mkuu wa Klabu ya Simba, Haji Manara ameamua kutumia busara zake kwa kumshauri Rais wa Shirikisho la soka nchini Tanzania (TFF), Jamal Malinzi kuwa zawadi ya mfungaji bora wa mwaka haikutakiwa kugawiwa kwa wachezaji wawili bali ingetumika njia ya kitalaam kumpata mchezaji anaestahili kupata kiatu hicho cha dhahabu.

Jamal Malinzi Kushoto na Haji Manara

Haji Manara baada ya kuona Posti ya Malinzi iliyotaarifu kuwa zawadi ya mfungaji bora msimu huu itaenda kwa wachezaji wawili waliofungana idadi sawa ya Magoli, amesema Tuzo ya kiatu cha mfungaji bora wa msimu huwa hakigawanywi badala yake TFF wangeangalia mchezaji mwenye Assist nyingi na idadi ya mechi alizocheza na aina ya magoli aliyofunga.

Kaka Rais tuzo hii huwa haigawanywi,angalia mwenye assist nyingi,dak na mechi walizocheza,idadi ya magoli yao kuna penati ngapi,nidhamu yao uwanjani,wenye ndiki yao ndio wafanyavyo hvyo kaka Rais, huo ni ushauri tu,ukiona vp niachie mwenyewe kaka Rais“ameandika Haji Manara.

Mapema leo Rais wa (TFF) Jamal Malinzi ametoa taarifa kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii akisema tuzo ya kiatu cha mfungaji bora itaenda kwa wachezaji wawili ambao ni Abdulrahman Mussa wa Ruvu Shooting na Simon Msuva wa Yanga wote wana magoli 14.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents