Michezo

Haji Manara atolewa kifungoni

Kamati ya nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemuachia huru  Mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa Simba Sports Club, Haji Sunday Manara na sasa kuendelea na majukumu yake.

Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Abbas Tarimba amesema wamechukua uamuzi wa kuzindoa adhabu za wadau kadhaa kwa mujibu wa sheria.

Lakini akasisitiza, adhabu ambazo hazikuwa na mashiko ni kusababisha chuki ndani ya mchezo wa soka jambo ambalo wasingelipenda.

“Lengo letu ni kuondoa chuki katika soka. Vizuri kuwa na umoja na watu wanaoshirikiana kwa ajili ya kuukuza mchezo wa soka badala ya kulalamikiana au kuchukiana,” alisema Tarimba aliyewahi kuwa mwenyekiti wa Yanga.

Tarimba alitangaza kufunguliwa kwa wadau kadhaa akiwemo Msemaji wa Simba, Haji Manara.

Manara alifungiwa kwa kutojihusisha na mchezo wa soka kwa muda wa miezi 12 na kutakiwa kulipa faini ya shilingi milioni tisa kwa utovu wa nidhamu wa kutoa matamshi yasiyo na stahiki kwa viongozi wa TFF pamoja na vyombo vya uongozi wa mchezo huo.

Pamoja na Manara, wengine walionufaika na uamuzi huo wa kamati ya nidhamu ni pamoja na Blassy kiondo ambaye ni kaimu katibu mkuu wa Chama cha Soka Rukwa. James Makwinya Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi Rukwa na Ayubu Myaulingo ambeye ni mwenyekiti wa Chama cha Soka Rukwa.

By Hamza fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents