Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Hanscana ajibu kuhusu ukimya wa Darassa

Ni miezi 10 sasa imepita bila ya kusikia ngoma mpya kutoka kwa Darassa huku ngoma yake ya mwisho ikiwa ni Hasara Roho, mashabiki wamebaki wakijiuliza nini kimemkuta? – Hanscana amejibu swali hilo.

Hanscana amekuwa karibu zaidi na rapper huyo huku akimsimamia katika baadhi ya kazi zake za muziki.

Akiongea na kipindi cha Chill na Sky kupitia Dizzim Online Hanscana amesema msanii huyo yupo poa na yeye mwenyewe ndio anajua kuhusu biashara yake ya muziki labda anajipanga ili kufanya vizuri zaidi.

“Nafikiria ni mipango tu, kilakitu kwenye maisha ni mipango. Darassa Muziki ni kazi yake ndio ofisi yake tusingeongelea Darassa bila ya kutaja muziki wake, labda tungeongelea mtu anaitwa Sharifu, Ramadhani au Hamisi,” amesema Hanscana.

“Naamini mtu mwenyewe ndio anajua kazi yake na mfumo wa biashara yake kuliko mtu yoyote yule. Mimi naamini vizuri Darassa anajua biashara yake na anajua muziki wake na kila kitu chake. Nadhani kila kitu anachokifanya kipo ndani ya mipango yake na anakiona zaidi hata ya sisi tunavyoona. Labda kuna kitu anakifanya muhimu, akija kuachia ‘Waooo’ ndio maana,” ameongeza.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW