Burudani

Harmonize aungana na Rayvanny; Ni baada ya A Boy From Tandale

Msanii wa muziki Bongo, Harmonize amesema kuwa yupo mbioni kutoa albamu yake.

Muimbaji huyo kutokea WCB ameiambia Bongo5 kuwa analazimika kutoa albamu kwa sababu ndio utambulisho rasmi wa msaniii ndani ya tasnia ya muziki.

“Nipo ndio nashughulikia albamu yangu lakini nipo kwenye hatua za mwisho sana, so muda wowote naweza kuitangaza lini itatoka, itakuwa na wasanii tofauti tofauti,” amesema Harmonize.

March 02, 2018 wakati Rayvanny akihojiwa na BBC Swahili alisema albamu yake ipo tayari na itakuwa inahusisha wasanii wengi kutoka Afrika.

Hadi sasa ni msanii mmoja pekee aliyetoa albamu ndani ya label ya WCB ambaye ni Diamond Platnumz. March 14, 2018 ndipo alipoizindua albamu hiyo ‘A Boy From Tandale’, Nairobi nchini Kenya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents