Michezo

Harusi ya Lionel Messi kufuru (Video+Picha)

Mchezaji wa timu ya taifa ya Argentina na klabu ya Barcelona, Lionel Messi amemuoa mpenzi wake wa muda mrefu, Antonela Roccuzzo hapo jana katika hoteli ya kifahari ya Rosario nchini Argentina.

 

Lionel Messi akiwa na mkewake, Antonela Roccuzzo

Messi mwenye umri wa miaka, 30 na mkewe Antonela Roccuzzo , 29 wamekuwa wapenzi tangu utotoni huku familia zao zikiwa majirani.  Harusi hiyo ya mchezaji bora wa dunia ilikuwa na wageni waalikwa 260 pekee huku maelfu ya askari polisi wakitanda maeneo hayo ya harusi.

Lionel Messi akiwa na mkewake, Antonela Roccuzzo

Messi alikutana na Roccuzzo akiwa na umri wa miaka 13 kabla ya kuhamia Hispania.

Mama yake Messi Celia, baba yake Jorge na dada yake Maria wakifika kwenye harusi ya Messi

Miongoni mwa wageni waalikwa hapo jana siku ya Ijumaa nipamoja na Luis Suárez, Neymar, Gerard Piqué akiwa na mkewe Shakira, wageni wengi wali wasili na ndege binafsi, magazeti ya nchini Argentina yameandika kuwa hiyo ni arusi ya mwaka.

Xavi Hernandez, Cesc Fabregas na Carles Puyol wakiwasili na wakezao

Mchezaji wa Argentine Ezequiel Lavezzi akiwa na Latina katika red kapeti

Rosario Hotel City Center ikiwa imeandaliwa kwaajili ya shukhuli hiyo

Mchoraji, Lisandro Urteaga akichora picha ya Messi katika ukuta Rosario huku ndoa ikiwa inaendelea 

Wananchi wakiwa nje ya hoteli ya Rosario wakitaka kushuhudia kinachoendelea

By Hamza fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents