Habari

Hataki kuimba kwa sababu hawezi kukata mauno

Zay BMsanii wa muziki wa kizazi kipya aliyewahi kuwa juu ile mbaya katika medani ya muziki hapa nchini Bi Zainabu Lupangile a.k.a Zay B amedai kuwa hawezi kufanya muziki wenye mahadhi ya kuimba kwa kuwa yeye hawezi kukata mauno

Zay B

 

Msanii wa muziki wa kizazi kipya aliyewahi kuwa juu ile mbaya katika medani ya muziki hapa nchini Bi Zainabu Lupangile a.k.a Zay B amedai kuwa hawezi kufanya muziki wenye mahadhi ya kuimba kwa kuwa yeye hawezi kukata mauno na ndio maana anakomaa na michano.

 

{xtypo_quote_left}Kiuno changu kigumu jamani Eh! – Zay B{/xtypo_quote_left} Kali hii ilitolewa na mkali huyo baada ya baadhi ya mashabiki ambao wameonekana kumuonea huruma kutokana na kupotea kwake kwenye gemu na kumtaka labda abadilike ajaribu kuimba kidogo pengine inaweza kuwa zali yake walau akatoka.

 

“unajua mashabiki ndio wananiletea michongo hiyo, eti wananitaka nibadilike na mimi niimbe kama wanafyofanya wasanii wenzangu wa kike lakini nasikitika kuwa siwezi kuwaridhisha katika hilo nikiwa na maana sitaweza kuimba kwani kiuno changu ni kigumu siwezi kukatika, pia nitaendelea kuchana kwani nimeshazoea pia ndio aina ya muziki unaonivutia, nisngependa kuwachekesha walionuna kwa mimi kuwa kioja kwenye jamii” alisema Zay To Tha B.

 

Msanii huyu amewahi miongoni mwa wasanii waliowahi kuwa tushio kwenye muziki wa bongo fleva hapa nchini lakini kwa sasa inavyoonekana kama ngoma yake imekuwa ngumu japo amejaribu kuchomoka na jiwe lake Odinali ambalo ameshirikiana na Banana Zoro.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents