Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Hatma ya Liverpool kwenye michuano ya UEFA Champions League hatua ya makundi baada ya kupoteza mchezo wa jana jioni

Hatma ya Liverpool kwenye michuano ya UEFA Champions League hatua ya makundi baada ya kupoteza mchezo wa jana jioni

klabu ya Liverpool wengi wakizoea kuiita Majongoo wa Anfield jana siku ya jumanne imepata matokeo mabaya kabisa katika michuano ya UEFA Champios league kwa kupoteza ugenini kwa jumla ya goli 2 – 0.

Liverpool jana walicheza na timu ya Fudbalski klub Crvena zvezda kwa kiingereza likimaanisha Red Star kutoka nchini Serbia, Red Star ni klabu iliyoanzishwa miaka 73 iliyopita nikimaanisha mwaka 1945 tofauti na Liverpool ambao walianzishwa mwaka 1892,miaka 126 iliyopita nchini Uingereza.

Kuanzia mwaka 2010 ikiwa imeshiriki michuano hii mara mbili tu msimu huu 2018-19 na msimu 2016-17, huku Liverpool wakishiriki mara 7 tangu mwaka 2010 ikiikosa mwaka 2011-12 na 2014-14, katika mchezo wa jana jioni walikuwa mwiba kwa Majogoo wa Anfield Liverpool kwa kuinyuka mabao 2-0.huku mchezo uliopita Liverpool waliibuka na ushindi wa goli 4-0.

Hatma ya Liverpool katika michuano hii ikoje wakiwa katika kundi ambalo linasemekana ni moja ya makundi ya kifo yaani kundi gumu kwenye michuano hiyo:-

Licha ya Liverpool kuwa nafasi ya pili kwa alama 6 huku tofauti ya magoli dhidi ya Napoli ikitofautiana timu yeyote kwenye kundi hilo inaweza kuvuka hatua inayofuata kwani zinatakiwa kuvuka timu mbili tu katika kila kundi.

Haya ndio matokeo ya jana katika kundi hilo, Liverpool walipoteza kwa kufungwa goli 2-0 na Red Star,PSG wakipata suluhu dhidi ya Napoli 1-1.

Mchezo ujao Liverpool wanakutana na PSG na Napoli wakikutana na Red Star, kama Liverpool watapoteza mchezo huo ambao utafanyika nchini Ufaransa na Napoli wakashinda dhidi ya Red Star kwa maana hiyo Napoli watakuwa na alama 9 na PSG watakuwa na alama 8,Liverpool watabakia na alama zao 6 na mategemeo yao yatakuwa kwenye mchezo ujao dhidi ya Napoli ambao utafanyika nchini Uingereza.

Hapo ndio itakuwa hatima ya Liverpool kwani PSG watakutana na Red Star na katika mchezo huo PSG ananafasi kubwa ya kushinda dhidi ya Red Star na mchezo kati ya Liverpool dhidi ya Napoli utakuwa mgumu sana.

By Ally Juma.

 

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW