Habari

Hatutolipia ujenzi wa ukuta kati ya Mexico na Marekani – Rais wa Mexico

Rais wa Mexico, Enrique Peña Nieto alisema Jumatano huu kuwa nchi yake haitolipia ujenzi wa ukuta kati yake na Marekani, na hivyo kukinzana na madai ambayo Rais wa Marekani, Donald Trump ameyatoa.

Hata hivyo kwa mujibu wa CNN, Rais huyo hajasitisha ziara yake nchini Marekani iliyopangwa kufanyika wiki ijayo.

“Mexico haiamini katika ukuta, nimesema sana hili, Mexico haitolipia kwa ukuta wowote,” alisema kwenye video aliyoiweka kwenye Twitter.

Peña Nieto amesema anasubiri ripoti ya mwisho kutoka kwa maafisa wake wa juu waliowasili Washington Jumatano hii kukutana na uongozi wa Trump.

Trump amependekeza kuwa sehemu ya dola bilioni 25 wanazopewa wahamiaji kila mwaka zitumike kujengea ukuta, jambo ambalo Mexico inapinga.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents