Michezo

Haya ndiyo atakayo fanyiwa Lengend wa Everton FC, Leon Osman kabla ya mchezo wao na Gor Mahia – Bodi ya Utalii

Kuelekea mchezo wa kirafiki baina ya klabu ya Everton FC ya nchini Uingereza ambayo inadhaminiwa na kampuni ya kubashiri michezo ya SportPesa dhidi ya Mabingwa wa SportPesa Super Cup timu ya Gor Mahia ya nchini Kenya mchezo utakao chezwa Julai 13 mwaka huu uwanja wa Taifa.

Viongozi wa SportPesa (katikati0 ,Bodi ya Utalii (kulia)  na Shirikisho la Soka nchini TFF (kushoto)

Bodi ya Utalii nchini yapanga mapokezi makubwa kwa mchezaji mashuhuri wa klabu hiyo ya Everton, Leon Osman ambaye atatangulia kufika nchini kabla ya timu yake kuwasili.

Akizungumza jana meneja wa bodi ya utalii nchini, Gofrey Meene alisema ujio wa Everton unaashiria kwamba Tanzania ni nchi salama na wenye watu wakarimu ambao wanaweza kuwa wenyeji wa timu kubwa kama Everton, na kuongeza ujio wao pekee unaitangaza nchi licha ya vivutio na sisi tunaona hiyo ni fursa.

 

“Kuja kwao kunavitu vingine vingi tu vitapata faida kama vile usafiri mahoteli vyakula sehemu wanapo kaa wote ni faida kwa hii timu tu kufika kwa hiyo kwa Tanzania kipato kinaongezeka na kila sekta ambayo inahusisha na ujio wao watafaidi,” alisema Meena.

Everton itafika nchini Julai 12, mwaka huu na siku hiyo wataenda kutoa somo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa wanafunzi wanaosomea michezo.

 

Tiketi 4000 zitatolewa kwa ajili ya kuingia uwanjani kuishuhudia Everton ikicheza na Gor Mahia, hizi tiketi zitawahusu wateja wa SportPesa wanaobashiri michezo kupitia kampuni hiyo.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents