Michezo

Higuain atua Chelsea kwa mkopo, ahaidi makubwa

Chelsea imemsajili kwa mkopo mshambuliaji wa Juventus Gonzalo Higuain mpaka mwisho wa msimu huu.

Miamba hiyo ya London pia ina nafasi ya kumsajili moja kwa moja kwa kima cha pauni milioni 31.3. Kuna uwezekano pia wa kuongeza mkataba huo wa mkopo mpaka Juni 2020 lakini itawapasa kutoa kitita cha pauni milioni 15.

Higuain, 31, ambaye ni raia wa Argentia amecheza nusu ya kwanza ya msimu huu kwa mkopo katika klabu ya AC Milan, na kufunga magoli nane kwenye michezo 22.

“Pale fursa ya kujiunga na Chelsea ilipojitokeza ilinibidi niichangamkie,” amesema Higuain.

“Ni timu ambayo nimekuwa nikiipenda na ina historia pana, uwanja mzuri na inashiriki Ligi ya Premia ambayo nimekuwa niiitamani kila siku kuicheza.”

Kutokana na usajili huo kufanyika baada ya saa sita usiku ya Jumatano, Higuain hataweza kuichezea klabu yake mpya kwenye mechi ya nusu fainali ya pili ya Kombe la Corabao usiku wa leo dhidi ya Tottenham.

Streka huyo alicheza chini ya kocha wa sasa wa Chelsea Maurizio Sarri katika klabu ya Napoli msimu wa 2015-16, na kufikia rekodi ya kutikisa nyavu kwa wingi katika ligi ya Serie A baada ya kufunga mabao 36.

“Ni mshambuliaji mwenye nguvu, alidhihirisha hilo katika msimu wangu wa kwanza na Napoli,” amesema Sarri. “Alifanya vizuri mno. Kwa hakika, yeye ni moja ya washambuliaji magwiji zaidi ambao nimewahi kufanya nao kazi.


Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents