Hii ndio Idadi ya Magoli aliyofunga Ronaldo Ukilinganisha na washambuliaji wa Juventus kuanzia mwaka 2006

Idadi ya magoli aliyofunga Cristiano Ronaldo katika ligi ya Mabingwa barani ulaya UEFA Champions League kuanzia mwaka 2006-2007 akiwa anaitumikia klabu ya Manchester United hadi hivi sasa alipoamua kuiaga klabu yake ya Real Madrid na kujiunga na Juventus.

Magoli 109 idadi kubwa ukiliganisha na Wafungaji 16 wa klabu ya Juventus waliofunga magoli kuanzia mwaka huo 2006-2007 hadi hivi sasa Ingawa wengine wameshastaafu na wengine wamehama katika klabu hiyo ya Turin.Jumla ya magoli yao ni 102 yakishindwa kuifikia idadi Ronaldo licha ya kufungwa na wafungaji tofauti 16.

Anayeongoza kwa wafungaji hao wa Juventus ni Higuain akiwa na magoli 10,Mandzukic goli 9,Tevez goli 7,Morata goli 7,Dybala goli 6,Quagliarella goli 6,Del Piero goli 5,Iaquinta goli 4,Llorente goli 3,Matri goli 2,Vucinic goli 2,Giovinco goli 2,Trezeguet goli 1,Bernardeschi goli 1,Zaza goli 1,na Amouri goli 1.

Ronaldo peke yake amefunga magoli 109 hiyo ndio tofauti ya Magoli ya Cristiano Ronaldo na wachezaji wa Mabibi kizee wa Turin Juventus ambaye rasmi kuanzia sasa ataanza kuvaa jezi yenye rangi ya Pundamilia inayotumiwa na Juventus akiwa mchezaji halali wa mabibi kizee hao baada ya kujiunga nao julai 10 2018 kwa ada ya Uhamisho inayofikia Euro Milioni 105.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW