Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Hiki ndicho kilichomchanganya Papii Kocha baada ya kutoka jela

Muimbaji wa muziki Papii Kocha amefunguka kitu ambacho kimemchanganya baada ya kutoka gerezani walipokuwa wamefungwa kwa takriban miaka 13 yeye na baba yake Nguza Viking maarufu kama Babu Seya.

Akiongea na kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM, Papii amesema alipoyaona magari ya Mwendokasi baada ya kutoka gerezani ndio yamemchnanya sana.

“Nimetoka nimekuta mambo mengi yamebadilika sana haswa mitandao hii, Kilichonichanganya zaidi ni mwendokasi natamani sana kupanda, pia nikitembea kwa miguu daah watu kila mahali Papiii Papii mambo yamebadilika sana,” amesema muimbaji huyo.

Papii na Babu Seya walifanikiwa kutoka gerezani kwa msamaha wa Rais John Magufuli kwenye maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania Bara mwaka jana.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW