Michezo

Hiki ndo kikosi bora cha Euro 2016 kilicho tajwa

Baada ya michuano ya Euro 2016 kumalizika na timu ya taifa ya Ureno kutwaa Kombe hilo, July 11 2016 shirikisho la soka barani Ulaya UEFA limetaja majina ya wachezaji 11 bora wanaounda kikosi bora cha Euro 2016.

Mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo, ni miongoni mwa wachezaji walioorodheshwa kwenye kikosi bora cha michuano ya Euro 2016 kilichotangazwa na Shirikisho la Soka Ulaya, Uefa.

Ronaldo aliwahi kujumuishwa katika kikosi cha mwaka 2004 na mwaka 2012.

Pepe pia yupo kwenye kikosi hicho na aliwahi pia kujumuishwa 2008 na 2012.

Awali, kulikuwa kukitajwa kikosi cha wachezaji 23 lakini wakati huu kumetajwa kikosi cha wachezaji 11.

Kikosi kamili kinajumuisha (4-2-3-1): Rui Patrício (Ureno); Joshua Kimmich (Ujerumani), Jérôme Boateng (Ujerumani), Pepe (Ureno), Raphaël Guerreiro (Ureno); Toni Kroos (Ujerumani), Joe Allen (Wales); Antoine Griezmann (Ufaransa), Aaron Ramsey (Wales), Dimitri Payet (Ufaransa); Cristiano Ronaldo (Ureno).

tott

Kikosi hicho kiliteuliwa na jopo la kiufundi la Uefa wakiwemo makocha, Sir Alex Ferguson na David Moyes.

“Tunaamini kikosi hiki cha wachezaji XI kinawakilisha wachezaji bora zaidi walioshiriki michuano,” amesema, Ferguson, ambaye ni balozi mwema wa ukufunzi wa Uefa.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents