DStv Inogilee!

Hili ndio gari lenye bei ghali zaidi duniani, gharama yake inazidi bajeti ya mwaka ya wizara ya habari

Kampuni ya kutengeneza magari ya nchini Ufaransa ya Bugatti, wiki iliyopita imezindua gari lake jipya la kwanza lenye gharama kubwa zaidi duniani kwa muda wote.

Image result for Bugatti La Voiture Noir

Bugatti La Voiture Noir

Gari hilo aina ya Bugatti La Voiture Noir ndio gari la gharama kubwa hadi sasa mwaka 2019, ambapo linauzwa kwa Dola Milioni $19 sawa na Tsh Bilioni 44 bila kodi.

Gari hilo ambalo tayari limeshanunuliwa na mteja mmoja kutoka Ujerumani, limetengenezwa maalum kwa ajili ya kusherehekea miaka 110 ya kampuni ya hiyo.

Gari la Bugatti La Voiture Noir limevunja rekodi ya kuwa gari lenye bei ghali zaidi duniani, rekodi hiyo awali ilikuwa inashikiliwa na gari aina ya Rolls-Royce Sweptail, lililokuwa linauzwa Dola Milioni $13 Sawa na takribani Bilioni 30 za Kitanzania.

Rolls-Royce Sweptail

Rolls-Royce Sweptail

Gari hilo ambalo tayari limeshanunuliwa na mtu mmoja kutoka Ujerumani, ambaye hakutaka jina lake litajwe, bado halijatajwa sifa zake ikiwemo spidi.

Tazama orodha ya magari yenye bei ghali zaidi duniani kabla ya toleo hili jipya kutangazwa.

ModelPrice
 Rolls-Royce Sweptail $13 million
 Mercedes-Benz Maybach Exelero$8 million
 Koenigsegg CCXR Trevita$4.8 million
 Lamborghini Veneno$4.5 million
 W Motors Lykan Hypersport$3.4 million
 Limited Edition Bugatti Veyron by Mansory Vivere $3.4 million
Ferrari Pininfarina Sergio$3 million
 Bugatti Chiron$2.9 million
Laferrari FXX K$2.7 million
Aston Martin Valkyrie$2.6 million
 Pagani Huayra BC$2.6 million
 Mercedes-AMG One$2.5 million
 Ferrari F60 America$2.6 million
 Aston Martin Vulcan$2.3 million
Milan Red$2.3 million
McLaren Speedtail$2.2 million

Gharama za gari hilo yaani Tsh Bilioni 44 ni nyingi kuzidi Bajeti ya mwaka wa fedha 2018/19 ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambayo ilikuwa ni Tsh Bilioni 33.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW