Technology

Hili ndio gari linalokimbia zaidi duniani, Kasi yake ni zaidi ya ndege ndogo (+Video)

Muda unakwenda kasi sana na teknolojia nayo inazidi kukua kila siku. Kwasasa kama utakuwa na fedha kiasi cha Dola Milioni $5.5  na unahitaji kwenda kununua ndege aina Cessna 408 Sky Courier kwa ajili ya kusafiria. Achana na mpango huo kwani Kampuni ya Bugatti ya Ufaransa imezindua gari yake yenye kasi zaidi duniani kushinda hata ndege hiyo.

https://www.instagram.com/p/B18ikZpBkeP/

 

Rekodi hiyo ya gari lenye kasi zaidi duniani, Imevunjwa na gari aina ya Bugatti Chiron kwa kwenda kasi ya kilomita 490.5 kwa saa (490.5km/h) sawa na 304.8 M/h.

Taarifa iliyotolewa na Kampuni ya Bugatti Jana Jumatatu, Imesema kuwa wamefurahi kwa kuvunja rekodi hiyo ya kuwa gari la kwanza lilsilo la mashindano kuwa na kasi kubwa zaidi duniani.

Bugatti wamesema kuwa gari hiyo ina uwezo wa kukimbia kilometa 500 kwa saa (500km/h) ila changamoto inakuja kwenye matairi yake ambayo wameleeza kuwa yanaweza yakawaka moto.

Kuhusu changamoto hiyo, Wamesema wapo tayari kutafuta suluhisho kwani matairi ya sasa yanayotumika yametengenezwa na kampuni ya Michelin.

Dereva anayehusika na majaribio ya magari ya Bugatti,  Andy Wallace amesema wakati akiendesha gari hilo, Alikuwa anajiona mwepesi na bado angeweza kuongeza kasi kama gari isingetoa tahadhari ya matairi.

Awali rekodi ya gari yenye kasi zaidi duniani isiyo ya mashindano, Ilikuwa inashikiliwa na gari aina ya Ehra-Lessien ya kampuni ya Volkswagen ya Ujerumani. Gari hiyo ilikimbia Miles 300 kwa saa (482.7 km/h).

Gari hilo la Bugatti Chiron linauzwa dola milioni $3 sawa na Tsh bilioni 6.8 za kitanzania.  Na kasi yake inaizidi ile ya ndege ndogo aina ya Cessna 408 Sky Courier inayokimbia Kilometa 370 kwa sasa.

Image result for cessna skycourier

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents