Michezo

Hili ndio rungu la CAF kwa timu ya Yanga

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), limeipiga faini ya dola 5,000 Klabu ya Young African kwa kosa la kuchelewesha mchezo baada ya wachezaji wake kumzonga mwamuzi wakati mchezo wa kuwania kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho dhidi ya GD Sagrada Esperanca uliofanyika Angola Mei 18, 2016.

coupe-caf-dim

Uamuzi wa mchezo huo Na. 100 ulifanywa na Kamati ya Nidhamu ya CAF inayoundwa Mwenyekiti Raymond Hack – Raia wa Afrika Kusini na wajumbe Mustapha Samugabo (Burundi) na Gbenga Elegbeleye (Nigeria). Pia alikuwako Amina Kassem kutoka Sekretarieti ya CAF ambaye ni Mtawala katika Kitengo cha Nidhamu.

Katika mkutano huo uliofanyika Cairo, Misri – Makao Mkuu ya CAF, Julai 3, 2016, kamati ilipitia taarifa zote za mchezo na kufikia uamuzi wa kuipiga faini Young Africans.

Taarifa za mchezo zinasema, wachezaji wa Young Africans walionyesha utovu wa nidhamu kwa kumzonga mwamuzi na kumsukuma mara baada ya kutoa adhabu ya penalti kwa wapinzani. Kwa tukio hilo, mchezo huo ulisimama kwa dakika sita. Polisi waliingia uwanjani kudhibiti hali hiyo.

Kwa kosa hilo, Wachezaji wa Young Africans walivunja Ibara ya 82 inayozungumza utaratibu wa mawasiliano. Kwamba chama chochote cha mpira wa miguu, klabu, ofisa au mtu yoyote wakiwamo wachezaji, lazima waheshimu utaratibu za kuvumilia, uadiliufu na uanamichezo.

Kwa mujibu wa Kamati hiyo ya Nidhamu ya CAF, Young Africans ilistahili kutozwa faini ya dola 10.000 za Marekani kwa makosa ambayo si uungwana kwenye soka yaliyoonyeshwa na wachezaji wake.

Lakini kwa kuwa Young Africans haikuonyesha utovu wa nidhamu katika mchezo mingine ya kimataifa iliyofuata dhidi ya MOB ya Algeria na TP Mazembe ya DRC, imepunguziwa adhabu na sasa wametakiwa kulipa dola 5,000 za Marekani kama faini. Faini hiyo haina budi kulipwa mara moja. Na imetakiwa kuendelea kuwa na nidhamu, vinginevyo adhabu hiyo itawarudia.

Tayari Young Africans imepewa namba za akaunti ya CAF inakotakiwa kulipa, lakini pia imepewa fursa ya kukata rufaa kama wataona kuna haja ya kufanya hivyo. Muda wa kukata rufaa ni siku tatu baada ya kupewa taarifa hiyo kwa maandishi.

Source: tff.or.tz

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents