DStv Inogilee!

Hip Hop Haiuzi kutoka kwa Madee yamchefua Dogo Janja

Msanii wa muziki Bongo, Dogo Janja amefunguka ngoma ambayo hakuwahi kuipenda kutoka kwa Madee.

Dogo Janja ametaja ngoma ya Madee ‘Hip Hop Haiuzi’ kama wimbo ambao hakupendezwa nao kabisa pindi ulipotoka.

“Kipindi hiyo unatoka nipo chuga, nachana sana na masela. Nikaona huyo vipi, masela wanasema huyu waki labda hasije chuga, tutamfanyia kitu mbaya, ” Dogo Janja ameiambia Kwetu Flavour ya Magic FM.

Hata hivyo utakumbuka Madee ndiye alikuja kumtoa Dogo Janja kimuziki. Wimbo wa kwanza wa Dogo Janja ndani ya Tip Top Connection uitwao Anajua Madee alifanya back vocal huku Tunda Man akisimama upande wa Chorus.

Madee kwa sasa anamsimamia Dogo Janja kupitia Manzese Music Baby (MMB) ambayo ni menejimenti iliyozaliwa ndani ya Tip Top Connection, pia inaelezwa albamu yao ya pamoja inayokwenda kwa jina la Mado imekamilika.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW