Michezo

Hivi ndivyo unavyoweza kushinda tiketi na SportPesa ya kwenda Uingereza kushuhudia mechi za EPL

Kampuni ya kubashiri matokeo ya SportPesa kushirikiana na gazeti la Mwanaspoti na Azam TV wamekuletea promosheni ya kujishindia tiketi za kwenda kushuhudia mechi za ligi kuu England msimu huu.

Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa SportPesa Tanzania, Abass Tarimba (katikati) akiwa na mfano wa tiketi.

Ukiachana na mamilioni wanayopata washindi kutokana na kupatia ubashiri wa mechi mbalimbali kupitia SportPesa, pia zile BET ID zitawapa ushindi mwingine wa kwenda Uingereza kushuhudia mechi za EPL.

Jumla ya washindi 8 watanufaika na dili hilo ambapo kila wiki mshindi mmoja atapatikana kupitia kampeni ya ‘Zali La Mwanaspoti’ inayoendeshwa na Gazeti la michezo la Mwanaspoti.

Wateja wanaobashiri na SportPesa wanatakiwa kununua Gazeti la Mwanaspoti na kujaza kuponi ambayo amepewaka katika gazezi la siku hiyo ambayo amebashiri.

Kuponi hiyo itahitaji mtu anayejaza awe ana BET ID aliyopewa baada ya kumaliza kubashiri mechi za siku husika kupitia SportPesa huku BET ID ikiwa ni ile uliyobeti siku husika ambayo gazeti limengia mtaani.

Pia mteja atatakiwa kujaza taarifa zake kamili pamoja na namba zake za simu na kisha kuipeleka kuponi hiyo kwa muuza magazeti.

Kwa maelezo zaidi tembelea katika mitandao ya kijamii ya SportPesa upate maelezo zaidi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents