Habari

Spika Ndugai amfagilia Dk Kashililah

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai ametoa shukrani kwa aliyekuwa Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah kwa utumishi mzuri ambao hautasahaulika.

 

Spika Ndugai katika picha ya pamoja na Katibu Mpya wa Bunge Ndg. Kagaigai (kushoto)na aliyekuwa Katibu wa Bunge Dkt Kashililah (kulia)

Spika Ndugai ametoa shukrani hizo leo,  Ikulu jijini Dar baada ya kuwaapisha  Mawaziri na  Manaibu na Katibu mpya wa Bunge.

“Ninyi mnatokana miongoni mwetu katika nyumba ile ya wabunge. Rais ameona awape nyadhifa hizi, kubwa na la kipekee nimkaribishe Katibu wa Bunge mpya Kagaigai na kipekee nimshukuru Dk Kashililah, asante sana kwa utumishi uliotukuka hatutakusahau,” amesema Spika Ndugai.

Rais Magufuli Oktoba 7 mwaka huu alimteua,Katibu wa Bunge mpya, Stephen Kagaigai na leo amemuapisha rasmi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents