Michezo

Hivi ndivyo Wa-Argentina walivyolichangamsha jiji la Madrid katika mchezo wa River Plate dhdi ya Boca Juniors (+Picha)

Usiku wa kuamkia leo ulifanyika mchezo wa kukata na shoka kati ya timu mbili kutoka nchini Argentina ambazo ni River Plate na mahasimu wao Boca Junior, ambao ulikuwa mchezo wa fainali raudi ya pili.

Mchezo huo ambao ulifanyika katika jiji la Mdrid na kuutumia uwanja wa Real Madrid ulikuwa wa pili baada ya mchezo wa kwanza uliochezwa Arggentina kutoa matokeo ya sare ya 2-2 lakini mchezo wa marudiano fujo zilitokea na baadhi ya wachezaji wa Boca Junior kuumizwa vibaya hivyo kuahirishwa na kubadilishwa kabisa mpaka uwanja utakaotumika katika mchezo wao wa pili, na badala yake kuletwa katika dimba linalotumiwa na klabu ya Real Madrid ambao unajulikana kwa jinala Santiago Bernabu.

Mchezo huo uliweza kuhudhuriwa na mastaa mbalimbali wanaotoka nchini Argentina na hata wanaotoka barani Ulaya na Afrika mpaka Asia, hii ni kutokana na uhasama uliopo kati ya hizi timu mbili.

 

Baadhi ya wachezaji waliohudhuria katika mchezo huu ni pamoja na Lionel Messi, Paul Dybala, James Rodriguez, Antonio Greizmain Falcao lakini pia kocha wa Atletico Madrid Giego Simion, na wengineo wengi.

Matokeo ya mchezo huu yalikuwa 3-1 ambapo River Plate walifanikiwa kushinda mchezo huo na kufanya aggregate kuwa 5-3 , Ikumbukwe kuwa dakika 90 za mchezo zilimalizika kwa timu hizi kutozana nguvu sawa baada ya sare na 1-1 na muda wa nyongeza ndipo hali ilipobadilika kwa upade wa Boca Junior baada ya kutandikwa goli zingine 2.

Mbali na mchezo huo kitu kingine kilichovutia ni jinsi aina ya mashabiki wa Ki Argentina wanavyopenda soka, katika jiji la Madrid walijaa wao tu na kufanya maandamano ya amani katika kila kona ya mji huo lakini balaa lilikuja pale ambapo River Plate walishinda taji hilo la Copa Libertadores.

By Ally Juma

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents