Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Hivi ndivyo wachezaji wa Leicester City walivyomuaga Boss wao Vichai Srivaddhanaprabha nchini Thailand

Hivi ndivyo wachezaji wa Leicester City walivyomuaga Boss wao Vichai Srivaddhanaprabha nchini Thailand

Baada ya mchezo wao dhidi ya Cardiff City siu ya jumamosi na kufanikiwa kupata ushindi wa goli mja amabo lilifungwa na Demarai Gray dakika ya 35 ya mchezo na kulidedicate goli hilo kwa aliyekuwa Boss wao ambaye aliaga maisha wiki iliyopita akitoka uwanjani baada ya Helcopiter yake kudondoka nje ya uwanja.

Baada ya goli hilo Gray alivua jezi yake na kuonyesha nguo ya ndani iliyoandikwa ” For Khun Vichai” baada ya goli hilo na ushindi huo jumamosi hiyo basi kesho yake siku ya Jumapili waliondoka nchini Uingereza na hadi nchini Thailand ili kuweza kuhudhuria mazishi hayo.

Timu nzima ya Leicester pamoja na uongozi wao akiwemo mtoto wa Vichai ambaye anaitwa Aiyawatt Srivaddhanaprabha nae pia alikuwepo kwenye huo msafara.

Jamie Vardy na nahodha wa klabu Wes Morgan ni miongoni mwa wachezaji ambao walihudhuria sherehe ya sala katika hekalu la Bangkok kwa mazishi ya Vichai Srivaddhanaprabha.

Baada ya mazishi hayo siku ya jumanne leo timu hiyo inatarajiwa kureje nchini uingereza ili kuendelea na ratiba zingine za ligi na kadhalika.

Wachezaji hao walijiunga na sala hiyo siku ya Jumapili kwenye hekalu la Budha kwa Mr Vichai na kufanya hivyo tena Jumatatu kabla ya kurudi nchini Uingereza siku iliyofuata kujiandaa kwa mechi yao ya nyumbani dhidi ya Burnley Jumamosi.

Shirika la habari la AFP lilisema kuwa wakati wa kuingia hekaluni, wachezaji waliifuata familia ya Bw Vichai na kukumbatia, kisha wakatoa maua ya jasmine na walipiga magoti mbele ya urn octagonal jeweled iliyotolewa na mfalme.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW