Habari

Hizi hapa Shule 10 zilizo fanya vibaya zaid kidato cha sita, matokeo mengine yazuiwa

Baraza la Mtihani la Tanzania (NECTA) kupitia kwa Katibu Mtendaje wake, Charles Msonde limetangaza matokeo ya kidato cha sita leo Julai 13 huku kati ya hao 13 wakizuiwa matokeo kutokana na sababu kadhaa na wengine nane kufutiwa kabisa matokeo kwa sababu ya udanganyifu.

Jumla ya watahiniwa 83,581 sawa na asilimia 97.58 ya watahiniwa 86.105 waliofanya mtihani wa kidato cha sita mwezi Mei mwaka 2018 wamefaulu. Ufaulu huo ni sawa na ongezeko la asilimia 1.53 kutoka asilimia 96.06 mwaka jana.

Bonyeza hapa kutazama matokeo ya kidato cha sita

Ubora wa ufaulu kwa watahiniwa wa shule unaonesha kuwa jumla ya watahiniwa 72,866 sawa na 95.52% wamefaulu katika daraja la kwanza hadi la tatu wakiwemo wasichana 30,619 sawa na 95.92% na wavulana 42,247 sawa na 95.23%. Waliopata daraja la kwanza ni 8,168.

Hata hivyo baraza la Mitihani la Taifa limefuta matokeo yote ya watahiniwa wanane waliobainika kufanya udanganyifu, kati yao wanne wakiwa ni watahiniwa wa shule na wanne watahiniwa wa kujitegemea huku wengine wakishindwa kukamilisha mitihani yao kutokana na sababu za kiafya na hivyo kufanya mitihani nusu, watapewa nafasi ya kurudia mwaka unaofuata.

Wakati baraza hilo limezuia kutoa matokeo ya watahiniwa 13 wa shule ambao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya mitihani kwa baadhi ya masomo. Watahiniwa hao watapewa fursa ya kufanya mitihani hiyo mwezi Mei 2019.

Shule ya Sekondari Jangwani ni miongoni mwa shule 10 zilizofanya vibaya zaidi. Nyingine ni.
1.Forest Hill, Jang’ombe, Jangwani, St. James Kilolo, White Lake, Aggrey, Nyailigamba, Musoma Utalii, Ben Bella, Golden Ridge.

Katika watahiniwa 10 bora kitaifa kwa upande wa Sayansi, watahiniwa wanne ni wasichana na sita ni wa wavulana wakiongozwa na Anthony Mulokozi kutoka Shule ya Sekondari Mzumbe.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents