Burudani ya Michezo Live

Hizi hapa sifa 12 za simu kali kwa mwaka 2019

Tukiwa tunaelekea kufunga mwaka 2019, hatimaye upepo wa kisulisuli kwenye ulimwengu wa Teknolojia umetuletea matoleo mbalimbali ya simu pamoja na uboreshaji haswa kwa upande wa kamera.

Ni ukweli usiopingika, kuna sifa nyingi tumeziona japokuwa bado kuna nafasi kwa makampuni haya ya simu kujiongeza.

Baada ya kufanya tafiti fupi, watu wengi wana dukuduku wakingojea toleo jipya la matoleo ya CAMON kutoka kwa kampuni ya TECNO.

Hizi ndizo sifa 12 wadau wanazotegemea kwenye toleo jipya la CAMON kutoka TECNO:

 • Uwezo wa kamera kutambua mazingira unayopigia picha, Yaani Artificial Intelligence
 • Ukubwa wa kamera hadi MP20 kwa kamera ya nyuma
 • Ukubwa wa kamera hadi MP 10 kwa kamera ya mbele
 • Kamera 3 nyuma
 • Uwezo wa kuzoom hadi mara 5
 • Kamera ya mbele yenye nyuzi 120 kupiga selfie na vitu ama watu wengi
 • Uwezo wa kupiga picha ang’avu usiku
 • Kioo kikali aina ya AMOLED
 • Dizaini matata iliyoundwa na madini ya shaba
 • Uwezo wa kuchaji kwa dakika 10 kutumia siku nzima
 • Prosesa na RAM kubwa ya kuifanya simu yako iwe na kasi
 • Uwezo wa kujaza mafaili kibao

Tuambie maoni yako, kipi ungetarajia kiwepo kwenye hii simu mpya inayotarajiwa kudondoshwa hivi karibuni tarehe 23 Oktoba 2019. Pia usisahau kufuatilia kurasa rasmi za kampuni ya TECNO Mobile Tanzania kwenye mitandao ya kijamii kujua mengi zaidi juu ya ujio wa mwanafamilia mpya wa simu za TECNO Camon.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW