Michezo

Hizi ndio takwimu kati ya Manchester Untd Vs Arsenal kabla ya mchezo wao wa usiku

Ligi kuu nchini Uingereza PL ilianzishwa mnamo februari 20 mwaka 1992 miaka 26 iliyopita ambayo inashirikisha timu 20 na moja kutoka katika visiwa vya Wales.

Kabla ya kubadilishwa jina mwaka 1992 zamani ilikuwa inaitwa Football League First Division ambayo ilianzishwa mwaka 1888, na timu inayoongoza kutwaa taji hili ni Liverpool ambao walilitwa mara 18.

Kati ya hizo timu 20 Manchester United ndio inaongoza kutwaa taji hili ikilitoa mara 13, yaani mara nyingi zaidi ya timu yeyote inayoshiriki ligi hiyo ikifuatiwa na  Chelsea ambazo imefanikiwa kutwaa mara 4 pamoja na Manchester City ambao wao wamelitwaa mara 3 pamoja na Arsenal.

Katika michezo ya leo usiku ipo kadhaa huku usiku wa jana kukiwa kumechezwa michezo kadhaa.

Mmoja ya mchezo mkubwa ambao utachezwa leo siku ya jumatano ni kati ya timu mbili kubwa sana ambazo i Manchester United dhidi ya Arsenal, na katika mchezo huo zifuatazo ni takwimu zao.

Timu hizi zimekuta mara 52 Manchester ikifanikiwa kushinda mara 24, michezo 16 ikishinda nyumbani huku michezo 8 ikishinda ugenini, lakini kwa upande wa Arsenal wao wamefanikiwa kushinda michezo 13 na michezo 10 ikifanikiwa kushinda nyumbani na michezo 3 ikishinda ugenini, lakini michezo 15 timu hizi zikitosana nguvu sawa.

Ikumbukwe kwamba ikiwa ni wiki ya 15 tangu ligi hii kuanza msimu huu Arsenal wako nafasi ya 4 na Manchester United wako nafasi ya 8, pia United akishinda michezo 6 ikipoteza 4 na sare 4 ikiwa imeshinda bila kuruhusu goli michezo miwili na mchezo iliyoshinda magoli mengi ni dhidi ya Burnley magoli 2-0 na mchezo iliyofungwa goli nyingi ni dhidi ya Spurs goli 3-0. Kwa upande wa Arsenal wao wakishinda michezo 9 ikipoteza 2 na sare 3 ikiwa imeshinda bila kuruhusu goli michezo 2 na mchezo iliyoshinda magoli mengi ni dhidi ya Fulham magoli 5-1 na mchezo iliyofungwa goli nyingi ni dhidi ya Man city goli 2-0.

Manchester City ndio wako kileleni kwa kuwa na alama 41 Arsenal katika nafasi ya 4 na alama zao 30 huku United nafasi ya 8 na alama zao 22.

By Ally Juma.

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents