Aisee DSTV!

Hong Kong yaufuta muswada tata wa sheria, Serikali yasisitiza mipango hiyo haipo tena 

Kiongozi wa Hong Kong Carrie Lam amesema leo kuwa muswada tata wa sheria ambao ungewezesha watuhumiwa kupelekwa China bara na ambao umezusha mgogoro mkubwa wa kisiasa katika eneo la Hong Kong umefutwa

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la DW,  Lam amekiri kuwa pendekezo la  muswada huo lilikuwa anguko la aina yake kwa serikali ya Hong Kong.

Katika mkutano wa nadra na waandishi wa habari mjini Hong Kong, Lam amesema ingawa bado kuna wasiwasi juu ya nia ya serikali ya kuufuta muswada huo, amewataka raia wa Hong Kong waamini kwamba pendekezo la muswada huo halitojadiliwa tena na hakuna mipango ya kuurejesha mezani.

Katikati ya Mwezi Juni, Lam aliitikia miito ya waandamanaji kwa kuuondoa kwa muda muswada huo wa sheria lakini matamshi yake ya leo yameashiria kuwa serikali yake haina tena nia ya kuendelea na mjadala kuhusu kupitishwa kwa muswada huo.

“Nilisitisha mara moja zoezi la kufanyia marekebisho muswada ule, lakini bado kuna shaka shaka juu ya dhamira ya serikali au kuna wasiwasi kuwa serikali huenda ikaanzisha tena mchakato wa muswada huo bungeni.

Nataka nisisitize hapa, hakuna mipango hiyo, muswada huo umekufa” Lam amewaambia waandishi habari mjini Hong Kong.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW