Michezo

Hongera Young Africans kwa kutwaa Ubingwa – FIFA

Siku chache baada ya Ligi kuu Tanzania bara kumalizika na klabu ya Young Africans kutwaa kombe la ligi, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Duniani (FIFA), Gianni Infantino, Mei 24, mwaka huu alituma ujumbe Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuipongeza klabu ya Yanga kwa kutwaa ubingwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2016/17.


Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani, Gianni Infantino

Young Africans imetwaa Kombe hilo ikiwa ni mara tatu mfululizo na katika salamu za pongezi, Rais Gianni Infantino amesema ubingwa huo wa Young Africans ni kielelezo cha ushirikiano baina ya wachezaji, kocha, utawala, matabibu pamoja na mashabiki.


Mabingwa wa Ligi kuu Tanzania Bara, kikosi cha Yanga wakishangiria Ubingwa wa msimu 2016/17

Katika pongezi zake Rais Infantino ameishukuru Young Africans na shirikisho la mpira wa miguu la nchi TFF kwa kusadia kupeleka ujumbe chanya kwa jamii kuhusiana na mpira wa miguu.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents