Habari

Hospitali na vituo vya afya nchini vyapigwa marufuku kupiga muziki

Hospitali na vituo vya afya nchini vyapigwa marufuku kupiga muziki

Hospitali zote nchini pamoja na vituo vyote vya kutolea huduma za Afya zimepigwa marufuku kuonesha miziki katika maeneo yakutolea huduma na badala yake kutakiwa kuweka jumbe zinazohusu Elimu ya Afya kwa umma pindi wanapongoja kupata huduma.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile hapo jana wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma za afya katika ukumbi wa halmashauri ya Muleba katika Mkoa wa Kagera.
“Ni marufuku kwa hospitali zote kuonesha miziki katika maeneo yote ya utoaji huduma za afya” amesema Dkt Ndugulile.
Dkt. Ndugulile amemwagiza Mganga mkuu wa Wilaya ya Ngara DKt. Revokatus Ndyekobora kuhamasisha wananchi Juu ya umuhimu wa kuudhuria kliniki kwa mama mjamzito walau mara nne ndani ya kipindi cha ujauzito wake na kuhakikisha wanajifungulia katika vituo vya kutolea huduma za Afya.
“Tuongeze kasi katika kuhamasisha wakina mama wajawazito kuhudhuria kliniki na kwenda kujifungulia katika vituo vya kutolea huduma za Afya. Miundombinu tunaendelea kuboresha, Mkoa mzima tumeleta shilingi Bilion 5.9 kwaajili ya kuboresha vituo vya Áfya, viwili vikiwa katika Wilaya ya Ngara .”
Pia alisema kuwa Serikali inaendelea kuboresha sekta ya Afya nchini kwa kutoa pesa ya ujenzi wa vituo vya kutolea huduma za Afya na kuhamasisha ushirikishwaji wa wananchi katika ujenzi wa vituo hivyo (Forced account)
Kwa upande mwingine Dkt Ndugulile aliendelea kusema kuwa katika kuelekea kuboresha huduma za afya Serikali imeanzasha utaratibu wa kituo nyota kwa vituo vya Afya, hospitali na Zahanati, na kutoa maagizo kwa Halmashauri zote nchini kuhakikisha Asilimia 80 ya vituo vyake vyote vya kutolea huduma za Afya havishuki chini ya nyota tatu (3)
“Serikali imeanzisha utaratibu wa kutoa madaraja ya Ubora kwa vituo vyote vya kutolea huduma za Afya , tunaanzia nyota sifuri kwa maana Kwamba kiwango chako chá Ubora ni chá chini sana Mpaka nyota 5 ambacho kiwango chako ni chá juu sana, tunataka Asilimia 80 ya Vituo vyao vyote katika kila halmashauri visipungue nyota tatu” Alisema Dkt Ndugulile.
Mbali na hayo Dkt Ndugulile amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Ngara. Luten Kanali Michael Mtenjele Kuimarisha usimamizi katika ngazi zote za Wilaya ili kuweza kufikia Ubora wa huduma za afya kwa Asilimia 80 katika vituo vyake vyote.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents