Habari

Huduma za afya zisifungwe wakati wa zoezi la usafi – Waziri Mkuu

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa ngazi mbalimbali waweke utaratibu utakaoruhusu huduma za afya kuendelea kutolewa kwa wananchi katika maeneo yao hata kama zoezi la usafi la kila mwezi litakuwa linaendelea.

Katika taarifa iliyotolewa leo na ofisi ya Waziri Mkuu imesema kuwa, Serikali imeweka utaratibu wa wananchi kushiriki katika shughuli za usafi wa mazingira siku ya Jumamosi ya mwisho wa mwezi, zoezi ambalo linashirikisha watu wote wakiwemo wafanyabiashara na watoa huduma nyingine zoezi linalofanyika kuanzia saa 12.00 asubuhi hadi saa 4.00 asubuhi.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo Bungeni mjini Dodoma katika kipindi cha maswali ya PAPO KWA PAPO kwa Waziri Mkuu wakati akijibu swali la Mheshimiwa Abdallah Ulega mbunge wa Mkuranga.

Mheshimiwa Ulega alitaka kupata kauli ya Serikali kuhusu maeneo ya kutolea huduma mbalimbali zikiwemo za afya ambayo hufungwa wakati wa zoezi la usafi linalofanyika kila mwezi nchini, jambo linalosababisha kero kwa wagonjwa na wengine wenye dharula.

Waziri Mkuu amesema “Hospitali na maeneo mengine ya kutolea huduma za afya hayawezi kufungwa, viongozi wa maeneo husika waweke utaratibu mzuri utakaoruhusu huduma hizo ziendelee kutolewa bila ya kuathiri zoezi la usafi wa mazingira.”

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents