In African bend na safari za nje
Kuna makundi mengi ya muziki wenye radha wa aina yake, hivi sasa hayasikiki kabisa… leo nikapata shauku ya kulitembele kundi moja la In African Band lenye kambi yake Temeke Sound Craft, kujua mbona kimya ndipo nikaambiwa storii hii kwa ufupi.
Kwamba kwa sasa wapo kimya kutokana na safari nyingi za Asia na Ulaya, ambazo wanakwenda kimuziki. Mmoja wa wanamuziki wa kundi hilo Bizman, alisema kwamba hivi sasa wapo mazoezini kwaajili ya kukamilisha nyimbo mbili ambazo watazitoa hivi karibuni.
Alisema ila katika miezi ya hivi karibuni wanatarajia kuanza tena kwa safari zao, ambazo zinawachukua muda mrefu, kwakuwa wanakuwa wantembelea sehemu mbalimbali kwaajili ya kutoa burudani.
Bizman mwanamuzki mkongwe na mpigakinanda mashuhuri, hasa pale alipopiga kwenye wimbo wa Tid wa Zeze.
Figueiredo mpiga bezi wa In Africa
Huyu ni mwimbaji na mpiga hii sijui wanaita nini phone
Nurudin Alfan mkunguta solo, pale kati na kufanya mambo yawe sawa.
Pomp Du Dominic mzee wa magoma, ambaye akichanganya mpango mzima unaenda sawa. hebu mtizame kwenye nyimbo zao mbili tatu kama Kidege na nyingine,
Richard Mwanisawa, mpiga drams na mwingine hapa hayupo anaitwa Stiven William akiwa kwenye upande wa kuimba akishirikiana na Bizman