Habari

INDIA: Auawa kwa kosa la kukalia kiti na kula chakula mbele ya watu wa tabaka la hali ya juu, hatimaye kudaiwa kupigwa vibaya kama adhabu yakosa hilo 

Jamii ya wahindi wa tabaka la chini linalojukina kama Dalit linaomboleza kifo cha mmoja wao aliyeuawa kwa kosa la ”kukalia kiti na kula” mbele ya watu wa tabaka la juu katika kijiji cha Kot nchini India.

Jitendra

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Mwezi uliyopita kundi la wanaume wa jamii ya wahindi wa tabaka la juu lilidaiwa kumpiga vibaya mtu aliyefahamika kama Jitendra mwenye umri wa miaka 23 ili kumuadhibu lakini alifariki siku tisa baadae.

Hakuna hata mmoja kati ya mamia ya wageni waliohudhuria harusi hiyo aliyejitokeza kuelezea masaibu yaliyomkuta Jitendra siku ya April 26. Lakini polisi imesema wazi nini kilichotokea.

Chakula katika harusi hiyo kilipikwa na watu wa jamii ya tabaka la juu kwasababu watu katika kijiji hicho hawagusi chakula kilichopikwa na Dalit ambao zamani waliitwa “wasio guswa”.

“Mzozo uliibuka wakati chakula kilipokua kikipakuliwa kuhusu nani aliyekalia kiti,” afisa wa polisi Ashok Kumar alisema.Geeta Devi

Geeta Devi anasema alimpata mwanawe akiwa amejeruhiwa nje ya nyumba yao

Ameongeza kuwa kisa hicho kimerekodiwa chini ya sheria (kupinga udhalimu) – iliyotungwa kuzilinda jamii zilizobaguliwa kihistoria nchini India.

Watu wa jamii ya Dalits, wamekuwa wakibaguliwa kwa muda mrefu nchini humo na jamii za matabaka ya juu.

Wakazi wa kijiji hicho kutoka jamii ya Dalit wanadai kuwa Jitendra alipigwa na kudhalilishwa harusini.

Wanasema aliondoka katika sherehe hiyo akilia machozi, lakini aliviziwa na kushambuliawa tena hatua chache kutoka mahali hapo na kupigwa vibaya sana.

Mma yake Jitendra, Geeta Devi, alimpata akiwa amejeruhiwa karimu saa za asuhuhi.

“Huenda alilala hapo usiku kucha,” alisema huku akionesha mahali alipomkuta. “alikuwa na majeraha na alama kila mahali mwilini mwake. Nilijaribu kusema nae lakini hakuweza kunijibu.”

Kot village in Uttarakhand state

Dalit ni wachache wakilinganishwa na familia zingine katika kijiji cha Kot katika jimbo la Uttarakhand

Bi Geeta Devi, hajui ni nani aliyemuacha mwanawe nje ya nyumba yao. Alifariki dunia siku tisa baadae akipokea matibabu hospitali

Kifo cha Jitendra ni pigo kwa mama yake ambaye alimpoteza mume wake karibu miaka mitano iliyopita.

Kati ya familia 50 zinazoishi katika kijiji cha kina Jitendra, ni familia 12 ama 13 ndio wa tabaka la chini la Dalit.

Polisi imewakamata watu saba wanaoshukiwa kuhusika na kifo cha Jitendra lakini wote wamekanusha kuhusika na kisa hicho.

“Hii ni hujuma dhidi ya familia yetu,” alisema mmoja wa mwanamke ambaye baba yake, ndugu zake na wajomba zake wanatuhumiwa kutekeleza uovu huo.

“Kwanini baba yangu atumie suala l matabaka katika harusi ya Dalit ?” aliuliza mwanamke huyo.

Lakini jamii ya Dalit katika kijiji hicho ambao walishuhudia kifo cha Jitendra, wanapinga vikali madai hayo.Kundi la watu wa tabaka la juu katika kijiji cha Kot

Watu wa tabaka la juu katika kijiji hicho wamekanusha madai ya kuwabagua watu wa jamii ya Dalit

Wanasema Jitendra alipatikana na ugonjwa wa kifafa, lakini wanapinga uwezekano kuwa alitumia dawa kupita kiwango alichoshauriwa na daktari.

Licha ya machungu waliyo nayo, familia za wadalit katika kijiji hicho wamekuwa watulivu.

“Hii ni kwasababu wanategemea familia ya watu wa tabaka la juu kiuchumi,” mwanaharakati Daulat Kunwar alisema.

“Dalit wengi hawana ardhi na wao huwafanyia kazi majirani zao wa tabaka la juu. wanajua athari ya kupaza sauti kuhusu kisa hicho.”

Familia ya Jitendra tayari imeshuhudia athari hizo- Geeta Devi anasema kuwa wanashinikizwa kutosema ukweli kuhusu kile kilichotendeka.

“Wanaume fulani walikuja nyumbani kwetu kututisha,” alisema “Hakuna wa kutusaidia lakini haturudi nyuma hadi tupate haki yetu.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents