Habari

INDIA: Fahamu mapacha hawa watano ambao wanne wanatarajia kufunga ndoa siku moja

Dada wanne kutoka jimbo la South Dandian huko Kerala ambako walizaliwa siku moja, wameishi maisha yao yote pamoja katika nyumba moja na kula chakula cha aina moja huku wakiwa wanavaa nguo sare na hata shule walienda shule moja na kusoma darasa moja mpaka walipofika umri wa miaka 15.

pancharatna

Na sasa dada hao wanaenda kuolewa katika siku moja.

Mapacha hao wana kaka yao mmoja, ila walijulikana wadada hao wanne tangu wazaliwe na hata kwenye mitandao ya kijamii wana akaunti moja ambayo wanatumia wote kwa pamoja.

Hii ndio simulizi waliiambia BBC inayo wahusu mapacha hao watano, mmoja wakiume na wanne wakike ambao wanatarajia kufunga ndoa siku mmoja.

Siku ya harusi

Dada hao wanne, Uthra, Uthraja, Uthara, Uthama na kaka yao walizaliwa tarehe 18 Novemba 1995 na wanapanga kufunga ndoa mwakani April 26.

“Mazungumzo yetu kwa sasa nyumbani ni kuhusu harusi yetu. Tunaangalia kitamba gani tutanunua kwa ajili ya magauni yetu ya harusi. Lakini tutanunua kitambaa cha aina mmoja na rangi moja na mshoto mmoja,” Uthara.The five siblings cutting five different cakes

Kumbukizi ya siku ya kuzaliwa kwao huwa wana keki nyingi

Mmoja ni mwandishi wa habari na mume wake mtarajiwa ni ripota.

Harusi itakuwa ya kitamaduni – tamaduni mbalimbali duniani zitakuwa sehemu ya sherehe ya harusi.

Badala ya kila mmoja kuchagua mwenza wake, wazee wa familia walifanya juhudi za kuwachagulia watu wa kuwaoa.

Mama yao, Rema aliwasaidia watoto wake kuchagua watu wa kuwaoa katika mtandao.

Harusi za namna hiyo huwa zinajumuisha wapenzi ambao wana hali ya kielimu au uchumi inayofanana.

Nyota za maharusi huwa zinazingatiwa pia na historia ya familia zao.

Lakini hii si ndoa ya kulazimishwa, bwana na bibi harusi lazima waridhie wenyewe kila mmoja.

Siku ya mahari mwezi Septemba zimeshafanyika, lakini kati ya bibi harusi wanne, watatu wanafanya kazi katika daraja la kati.

Lakini hali ya wao kuwa mapacha haiwafanyi wao kuoneana tofauti na watahakikisha kuwa harusi yao itafanana kwa kitu.

Maisha yao yakoje

Katika maisha yao wamekuwa wakishirikiana karibu na kila kitu tangu wazaliwe, Licha ya kwamba si mapacha wa kufanana kabisa.Pancharatna quintuplets have scored excellent grades

 

Uthraja alifuuzwa shule. Uthama alipenda muziki na alijifunza kupiga vyombo vya muziki-‘ violin’, huku kaka yao r Uthrajan alikuwa anapenda kupiga vyomo vya muziki wa India.

Uthra aienda kusomea ubunifu wa nguo. Uthraja na Uthama walikuwa mafundi mitambo wa hospitalini.

Hivyo walivyoanza kutafuta waume zao, Uthraja alianza kwa kutafuta mwenza kwa mwaka mmoja uliopita, lakini aliamua kutokuwa na haraka.

Tunafurahia kusubiri

“Ni mama yetu ndiye alikuwa anatamani tuolewa siku moja . Hivyo tuliamua kusubiri,” Uthraja aliiambia BBC.

Kupanda harusi ya kihindi ni gharama sana, na harusi nyingi huwa zinajumuisha ndugu binamu au watu wa aribu wa familia kuwa na harusi ya pamoja ili kupunguza gharama.

Hivyo wadada hao wanne kupanga harusi ya pamoja, itaweza kumsaidia mama yao kifedha lakini dada hao wanafurahia hisia yao zaidi upande wa uchumi.

Kwa bahati nzuri mume mtarajiwa wa Uthraja, hakulazimisha harusi kufanyika mapema.

Yeye anaolewa na Akash Kumar, ambaye ni fundi mitambo kwenye hospitali katika daraja la tatu.

“Huwa tunafanya kazi pamoja katika hospitali moja kabla hajaenda Kuwait. Tunafahamiana na familia yake ilifurahi kuja kwa mama yangu,” alisema.

Hivyo anataka kumaliza miaka miwili katika ajira yake kabla hajahama nchi.

Hii ikiwa inamaanisha kuwa ataenda kukaa na mume wake miezi michache baada ya ndoa yao.

“Ni kitu kigumu kidogo na kinahuzunisha . Kuogopa kupo kwa sababu sijawahi kukaa katika nchi nyingine.Wakati huohuo nina shauku kubwa ya harusi yetu.”

Uthraja anatumaini kuwa itakuwa rahisi kupata kazi Kuwait – Uthra na Uthama pia wanaolewa na wanaume wa daraja la kati.

Mipango ya harusi hiyo itawasaidia kusahau machungu ya maisha waliopitia miaka iliyopita.Young kids enjoying a bit of sun light

Rema Devi anasema kuwa walizaliwa wakiwa na uzito mdogo

Wazazi wao walifurahi kupita kiasi kuwakaribisha duniani mapacha hao watano na nyumba yao wakaipa jina la”Pancharatna” – ikiwa ina maana ya vito.

Watoto hao walikuwa na maendeleo mazuri shuleni ingawa afya ndio ilikuwa mgogoro.

“Walizaliwa wakiwa na uzito mdogo na walikuwa wakiugua kila mara,” alikumbuka Rema Devi, mama yao.

Wazazi wao Prema Kumar na Rema Devi waisumbuka kuwalea watoto wao watano. Alihangaika sana na afya za watoto wao.uthraja

Kuwalea mapacha hao watano haikuwa rahisi kwa mama yao Rema Devi

Walikuwa na fedha kidogo ya chakula na walizingatia kwenye elimu zaidi .

Huko India mtoto wa kiume huwa wanapewa kipaumbele kikubwa.

Lakini wadada hao wanasema kuwa hali ilikuwa tofauti kwao walikuwa wanalelewa vizuri na kupewa kipaumbele katika familia kama watoto wa kiume.

Vilevile wadada hao walisema kuwa wazazi wao walipewa haki sawa, walinunuliwa nguo za kufanana na ikapelekea mara nyingine wavaliane nguo.

“Tulikuwa hatugombani, tulikuwa hatukasirikiani tukivaliana nguo,” alisema Uthara.Rema Devi with her husband

Rema Devi akiwa na marehemu mume wake wanadai kuwa na wakat mgumu kuwalea watoto wao

Baba yao alikuwa na duka la vifaa vya shule ndio lilikuwa chanzo cha kipato chao,Wakati watoto hao wana miaka 9, baba yao alipoteza pesa nyingi katika biashara yake na kuamua kujiua mwenyewe mwaka 2004.

Jirani yao ambaye ni daktari aliguswa na maisha yao hivyo aliamua kuwasaidia kwa kuwapa mahali pa kuishi na walishukuru sana kwa msaada huo.

“Hali ya shida inasaidia kupatikana kwa watu wazuri zaidi ,” alisema Rema Devi.

Watoto hao walihitimu masomo yao kwa ufaulu wa juu.

“Mama yetu anafuraha sana na anataka tuwe huru,” says Uthara.

Vyombo vya habari

Tukio la harusi yao itakayofanuika katika hekalu maarfu nchini India.Quads with their mum

Marafiki na ndugu wa karibu ndio watakaribishwa peke yake. Waandishi wa habari na wapiga picha watakuepo pia.

“Harusi hii itakuwa ya aina yake na baraka kubwa kwetu,” alisema Uthara.

Mitandao ya kijamii na vyombo vya habari vimeandika namna wadada hao waliozailiwa siku moja wanafunga ndoa siku moja.

Wadada hao wanafikiri namna gani wataendelea kukumbukana na wataendelea kumsaidia mama yao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents