Habari

Iran yaanza msako waliyodungua ndege ya Ukraine

Rais wa Iran Hassan Rouhani amesema wale waliohusika katika kuidungua ndege ya abiria ya Ukraine ni lazima waadhibiwe.

Image result for ukraine plane shot down

Katika hotuba iliyopeperushwa kwenye televisheni ya taifa rais huyo amesema wale waliofanya kosa hilo ni sharti wahukumiwe.

Ameongeza kwamba tukio hilo lililosababisha mauaji ya watu wote waliokuwa ndani ya ndege hiyo litafanyiwa uchunguzi wa kina ambapo ameitaka idara ya mahakama nchini humo kubuni jopo maalum lenye majaji wa ngazi ya juu na wataalam akidai kwamba ulimwengu utakuwa ukitazama.

Kwa mujibu wa chombo cha habari cha Deutsche Welle, Rouhani amesema pia kwamba ni kosa ambalo haliwezi kusameheka na kwamba haiwezekani kwamba mtu mmoja tu ndiye aliyehusika. Msemaji wa idara ya mahakama ya Iran amesema tayari kuna watu waliokamatwa kuhusiana na tukio hilo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents