Michezo

ITF yampunguzia adhabu Sharapova

Mcheza tenesi Maria Sharapova ambaye ni bingwa wa Grand Slam mara 5 ambaye alikuwa amefungiwa kucheza tenesi kwa miaka miwili, sasa amepunguziwa adhabu yake na chama cha tennis duniani ITF, mpaka kubakia miezi 15 na hivyo atarejea dimbani tarehe 26,April,2017.

maria-sharapova-retires

Sharapova amepunguziwa kifungo hicho baada ya kukata rufaa katika mahakama kuu ya michezo duniani.

Mrussia huyo,29, alifungiwa kufuatia kufeli vipimo vya madawa kwenye michuano ya Australia Open mwezi januari,2016 baada ya kugundulika ametumia dawa za Meldonium zilizozuiliwa katika michezo.

Meldonium,ni dawa za magonjwa ya moyo ambazo jina lingine ni Mildronate, zimezuiliwa kutumika tangu Januari,1, 2016

Sharapova ambaye aligundulika kutumia dawa hizo karibia mwezi mmoja tokea zilipofungiwa januari 2016.

Sharapova amesema kuwa alikuwa akitumia dawa hizo tangu mwaka 2006 kwa sababu za kiafya na hakufahamu kama zimekatazwa katika michezo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents