Burudani

Jason Derulo alizwa zaidi ya $300k

Msanii wa Marekani Jason Derulo amesherekea wikiendi hii kwa kumwaga machozi.

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, umeripoti msanii huyo amejikuta nyumba yake iliyopo mjini Los Angeles ikivamiwa na kuibiwa kiasi cha dola 300,000 pamoja na vitu vingine vya thamani kubwa. Hata hivyo msanii huyo hakuwepo nyumbani muda huo.

Inadaiwa kuwa mmoja wa wafanyakazi wake ndio aligundua hilo baada ya kuona mlango umefungwa na wakati huo huo dirisha likiwa limevunjwa wakati alipotembelea kwenye nyumba hiyo Ijumaa iliyopita.


Picha ya nyumba ya Jason Derulo iliyoipiwa

Polisi walifanikiwa kufika eneo la tukio lakini haikufahamika zaidi vitu vingine vilivyoibiwa, ndipo walipoamua kumsubiri Jason atakaporudi ili aweze kutambua vitu vingine vilivyoibiwa.

Wasanii wengine ambao wamewahi kupatwa na mkasa kama huo ni pamoja na Demi Lovato, David Spade, Kendall Jenner, Drake, Emmy Rossum, Alanis Morissette, Scott Disick na Nicki Minaj.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents