Habari

Je, wewe ni mlevi wa ngono?

Je wewe unahangaishwa na hisia za kutojitosheleza, kukosa usalama, unyonge? Wanasaikolojia husema kuwa watu wanaohangaishwa na hisia hizi kwa kawaida hutumia ngono kama njia ya kuzificha. Tunaweza kukubaliana kuwa ngono ni tatizo hapa Tanzania.

Utawakuta machangudoa wakijinadi hadharani kwenye migahawa, mabaa, vilabu na mitaani, na biasahara yao inatija!

Mbali na machangudoa, ninakumbuka kuongea na mvulana mmoja siyo muda mrefu uliopita ambaye jina lake limehifadhiwa. Bila shalka alikuwa kijana mzuri, mrefu, mwenye rangi nzuri, mtanashati; tatizo ni kwamba alifahamu kuwa ni mzuri.

Alikiri kuwa alifanya mapenzi na machangudoa, mara kwa mara. Nilishituaka sana, kijana ambaye angeweza kumpata msichana yeyote yule, na ambaye angelala naye bila kumlipisha chochote, alikuwa akiwalipa wanawake kupata ngono!

Hata hivyo, siyo kuhusu ngono tu, bali ni kiungo cha kihisisa kinachopatikana wakati wa kufanya mapenzi. Walevi wa ngono ni kama walevi wa madawa au pombe, na sawa na walevi wa madawa na pombe, mleviwa pombe hutafuta kwa bidii kubwa kutoka chanzo cha nje kutuliza maumivu ya ndani. Mawazo yao daima hutawaliwa na ngono na hawawezi kudumisha mahusiano salama na yeyote.

Nilipomuuliza rafiki yangu kisa cha kuwalipa malaya kupata ngono, yeye aliniambia kuwa hakuwa na budi ila kufanya hivyo, alishindwa kujizuia lakini hakuwa na jibu sahihi, dalili ya kwanza ya mlevi wa ngono.

Sawa sawa na walevi wengine, walevi wa ngono hukana kabisa kuwa anatatizo na hujaribu kutoa kisingizio na maelezo kuhusu tabia yao na aghalabu hulaumu kitu au mtu mwingine mtu anayeteswa na ulevi huu  kwa kawaida haridhishwi na tendo la ngono lenyewe na pia hajengi mahusiano na mwenzi wa mapenzi. Kwa kawaida hujihisi kuwa hawana uwezo wowote, na hawana mamlaka juu ya vitendo vyao hata kama wanajua matokeo ya vitendo vyao, ama vya kijamii, kifedha, au vya kiafya.

Baadhi ya dalili za mlevi wa ngono kufuatana na mtandao wa tiba medicinenet.com ni kama fuatavyo:
•    Hujisugua yeye mwenyewe au lugha ya mitaani hufanya punyeto. (kujisisimua)
•    Mahawara wengi (mahusiano nje ya ndoa).
•    Wapenzi wengi wasiojulikana pamoja na au pia na wale wa mpito tu
•    Matumizi ya kudumu ya picha za ngono
•    Ngono isiyo salama.
•    Ngono  kwa njia simu au kompyuta (ngono ya mtandao au cybersex)
•    Umalaya au kutumia makahaba
•    Kujionesha uchi
•    Kutpania kuafuta kujuana na wasichana au wavulana kupiia matangazo magazetini
•    Kuchungulia madirishani au kupiga chabo au bodi
•    Unyanyasaji wa kingono
•    Uchokozi wa kuumbua/ ubakaji

Hatua ya kwanza la kushinda tatizo hili ni kukiri kwamba tatizo lipo.ninajua kuwa hapa Tanzania, hatuna madaktari wa akili wengi, bali tunao viongozi wa kidini wengi ambao wamefundishwa kutoa ushauri nasaha kwa hiyo weak pembeni dini, mtafute mchungaji au kasisi na mweleze tatizo lako, au ikiwa unamfahamu daktari wa akili, nenda kaongee naye! Hapo umo njiani kupona.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents